Wednesday, January 26, 2011

MATOKEO KIDATO CHA NNE NJOMBE

MATOKEO KIDATO CHA NNE NJOMBE,WALIOHITIMU WAFULIKA KWENYE MIGAHAWA YA MAWASILIANO.

Mara baada ya baraza la mitihani nchini Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne waliofanya mtihani yao mwezi wa kumi mwaka jana,hali imekuwa ni ya kupishana kwenye migahawa ya mawasiliano kwa wanafuzi na wazazi wa watoto mbali mbali ili kuweza kujua matokeo hayo.

Mara baada ya baraza la mitahani Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne na kuyaweka katika mtandao wa baraza hilo,watahiniwa mbali mbali wamejitokeza katika migahawa ya mawasiliano kuangalia ufaulu wao kwa sehemu mbali mbali nchi.

Mara baada ya baraza la mitihani nchini Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne waliofanya mtihani yao mwezi wa kumi mwaka jana,hali imekuwa ni ya kupishana kwenye migahawa ya mawasiliano kwa wanafuzi na wazazi wa watoto mbali mbali ili kuweza kujua matokeo hayo.
Mtandao huu umefanikiwa kupita katika sehemu mbali mbali za migahawa hiyo ya mawasiliano kwa mji wa Njombe na imekuta idadi kubwa ya wanafunzi waliojitokeza katika kuangalia matokeo hayo yaliyotangazwa na baraza la mitihani hapa nchini.

Hali hii imekuwa ikiwapa wakati mgumu kwa wanafunzi kuweza kupokea matokeo yao mara baada ya kufanya mitihani yao mwezi wa kumi mwaka 2010 na kusubiri matokeo yao kwa kipindi chote cha takribani miezi mitatu.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa wanafuzi waliohitimu mwaka huo wa 2010 katika shule ya mpechi wilayani Njombe mkoani Njombe aliyekataa kutaja jina lake anasema matokeo ya mwaka huu kwa shule za serikali sio mazuri sana kutokana na shule za serikali kubwa na upungufu wa walimu ,vile vile kutokuwepo kwa vifaa vya ufundishaji ikiwemo vifaa vya maabara kwa nyingi za serikali.

Kijana huyu anasema kwa upande wake yeye matokeo yake hayajakuwa mazuri sana kama alivyokuwa akitarajia.

Ameongeza kuwa moja ya vitu ambavyo pia vimepelekea kuanguka kwao katika ufaulu ni pamoja na kitendi cha serikali kuondoa mtihani wa kidato cha pili hali inayopelekea kwa wanafunzi waliofanya vizuri na wasiofanya vizuri kuendelea katika kidato cha tatu hivyo kutowafanya wanafunzi wengi kutokuwa makini hali inayowapelekea kufika kidato cha nne wakiwa bado hawana uwezo mzuri kitaaluma.

Hata hivyo baadhi ya wazazi wilayani hapa wamesema kuwa ufaulu wa watoto wao wengi wao umekuwa si mzuri sana kutokana na watoto wao wengi waliokuwa shule za serikali kutokufanya vizuri kama wale wenzao wa shule za binafsi.

Mtandao huu haukufanikiwa kukutana na afisa elimu wa wilaya hii ya Njombe kuweza kuzungumzia ufaulu kwa wilaya ya Njombe na shule zake kwa ujumla.

Sunday, January 9, 2011

MENEJA WA KITUO CHA RADIO UPLANDS FM AFARIKI DUNIA.


KWA MASIKITIKO MAKUBWA NIKIWA KAMA MKURUGENZI MTENDAJI WA KITUO CHA REDIO CHA UPLANDS FM CHA HAPA MJINI NJOMBE NAOMBA KUWATANGAZIA KUWA ALIEKUWA MENEJA WA KITUO HIKI BWANA VITUSI THOMAS SWALE AMEFARIKI DUNIA JANA MAJIRA YA SAA KUMI NA MBILI JIONI KATIKA HOSPITALI YA MJINI NJOMBE KIBENA

 

KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU RATIBA YA MAZISHI NA MIPANGO YA MAZISHI MTAENDELEA KUFAHAMISHWA KUPITIA KITUO CHA RADIO CHA UPLANDS FM NA KUPITIA MTANDAO HUU PIA KADIRI MIPANGO YA MAZISHI INAVYIOENDELEA KUPANGWA

 

KWA NIABA YA FAMILIA YA SWALE,WAKURUGENZI WA UPLANDS FM,WAFANYAKAZI WA UPLANDS FM,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI TUNASEMA MUNGU AMEMPENDA ZAIDI BW VITUS THOMAS SWALE KULIKO UWEZO WETU KAMA WANADAMU.

 

TUNAWAOMBA KUWA WAVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU NA KWASIKILIZAJI WA UPLANDS FM TUNAOMBA KUWATANGAZIA KUWA VIPINDI VYETU HAVITOKUWA KATIKA UTARATIBU WA KAWAIDA KWA KIPINDI CHOTE CHA MSIBA HADI HAPO MTAKAPOTANGAZIA TENA BAADAE

Saturday, January 1, 2011

HAPPY NEW YEAR 2011

MTANDAO WAKO WA KIHABARI YAANI HABARIKWANZA,UTAKUTAKIA SIKUKU NJEMA ZA MWAKA MPYA WA 2011.WAANDAAJI NA WANAHABARI WA MTANDAO HUU KWA PAMOJA TUNAWATAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA MWAKA HUU WA 2011.KILA LAKHERI MTANZANIA NA MSOMAJI WA MTANDAO HUU........HABARIKWANZA........