Wednesday, February 9, 2011

SHIDA YA MAJI YAWA KERO,WAKAZI WA KIMARA

SHIDA YA MAJI YAWA KERO KWA WAKAZI WA KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM.


Tatizo la maji kwa wakazi wa jiji la dar es salaam limezidi kuwa kero kwa wakzi wengi wa jiji kufuatia kutopata huduma hiyo kwa kipindi kirefu sasa kwa maeneo mengi.

Hali hiyo imejidhihilisha kwa wakazi wengi wa maeneo ya kimara ambao ni kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa huduma hiyo imekuwa haipatikani katika maeneo yao hali inayosababisha hali ya maisha kuwa ngumu zaidi ya ilivyokuwa sasa.

Mtandaao huu uliwakikuta kina mama wengi wa maeneo hayo ya kimara wakiwa mamekusanyika katika bomba dogo lililokuwa likivuja ili kuweza kupata huduma hiyo ya maji.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti wakazi hao wa maeneo ya kimara wamesema shida ya maji imekuwa ni kero kubwa kwa upande wao hali inayowalazimu kutafuta maji kwa muda mrefu na pale wanapoyapata katika magari yanayouza maji hayo basi bei nayo imekuwa tatizo kwani ndoo moja ya lita ishirini imekuwa ikiuzwa kati ya shilingi mia moja na hamsini hadi mia mbili na hamsini hali inayowafanya washindwe kumudu gharama hizo.

Juhudi za kuwapata maafiasa wa DAWASCO kuweza kuzungumzia tatizo hilo hazikuzaa matunda na badala yake mtandao huu ulikutana na afisa mmoja aliyekataa kutaja jina lake kwa kusema kwamba yeye si msemaji,na kuongeza kuwa tatizo linalosababisha kukosekana kwa maji ni kupungua kwa presha katika mambomba hayo na pale yanapotoka watu wachache wamekuwa wakiyaaiba maji hayo kwa kuyavuta na mota kisha kupandisha katika matanki yao hali inayofanya maji kusambaa katika maeneo mengine.

Hali hii ya kukatika kwa huduma ya maji katika maeneo mengi ya jiji la dar es salaam imekuwa kero kwa wananchi wengi wa jiji hili ikiwa ni sambamba na kero ya kukatika kwa umeme,hali ambayo imekuwa ikiwasumbua wakazi wengi wa jiji hili.

Katika maeneo hayo hayo ya kimara kwa siku ya tarehe 8 mwezi huu wa pili (2) umeme nao ulikatika toka majira ya saa mbili za asubuhi na kurudi majira ya saa tatu na nusu za usiku hivyo kuwafanya wakazi hao kutokuwa na huduma ya maji na umeme katika maeneo yao.