Tuesday, April 16, 2013

NMB KANDA YA MASHARIKI YATOA MSAADA WA MADAWATI 38 YENYE THAMANI YA TSH MIL 2.5 KATIKA SHULE YA MSINGI MTYANGIMBOLE WILAYANI KILOMBERO

Zaidi ya
wanafunzi 80 wa darasa la nne na la
tano wa shule ya msingi ya
Mtyangimbole
iliyopo kijiji cha Ikule kata ya
Mngeta wilayani
Kilombero,wanasomea kwenye
banda la nyasi huku wakiwa
wamekaa chini.

HabariKwanza Blog imeshuhudia hali hiyo
wakati wa makabidhiano wa msaada
wa madawati
38 yenye thamani ya shilingi milioni
mbili na laki tano uliotolewa na
Benki ya
Nmb Kanda ya mashariki shuleni
hapo.

Akizungumzia
hali hiyo Mwalimu Mkuu wa shule
hiyo bwana Emanuely Njavike amesema
kuwa wamelazimka
kufanya hivyo kutokana na shule
hiyo kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa
kwani vyumba
vilivyopo kwa sasa ni
viwili ambavyo vinatumiwa kwa
kupokezana kwa darasa la kwanza,la
pili,la tatu
na la sita.

Mwalimu Njavike
amesema kuwa hali hiyo
imewafanya
wanafunzi kutohudhuria masomo
kikamilifu kutokana na miundombinu
ya shule hiyo
kuwa mibovu hususan kipindi hiki
cha masika ambapo maji hujaa
katika vyumba hivyo na kuwafanya
wanafunzi hao kusoma katika
mazingira magumu na hatarishi.

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha
Mtyangimbole Bwana Sangalufu John
Kibonde amesema
kuwa wananchi wa kitongoji hicho
walijenga maboma mawili mara
mbili na
yakabomoka kutokana na mvua za
masika
zinazoendelea kunyesha baada ya
serikali
kuchelewa kumalizia maboma hayo
hali inayowakatisha tamaa wananchi
kuchangia
ujenzi wa shule hiyo.
Shule ya
Mtyangimbole yenye wanafunzi 195
kuanzia
darasa la kwanza hadi la sita
inakabiliwa na upungufu wa vyumba
vitano vya madarasa na matundu
nane ya vyoo.

Hata hivyo maafisa wa benki ya NMB na Mbunge wa viti maalumu kupitia
Chama cha demokrasia
na maendeleo chadema Mheshimiwa
Suzan Kiwanga wamesikitishwa na
hali hiyo na
kusema kuwa shule hiyo inahitaji
msaada wa hali na mali ili
kuwanusuru watoto
hao wanaosoma katika mazingira
magumu na hatarishi

Monday, April 15, 2013

AJINYONGA KUEPUKA MADENI

MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la
Karimu Kamwenda(41) mkazi wa
Kitongoji
cha Michenga A kijiji cha Michenga wilayani Kilombero
amejinyonga usiku wa kuamkia
leo kwa kile kinachodaiwa ni kukwepa madeni.

Kwa mujibu Mwenyekiti wa Kijiji cha Michenga
Bwana Iddi Kamila ameiambia
habarikwanza
kuwa kwa maelezo ya Kaka wa
Marehemu huyo, kuwa Marehemu amejinyonga
kwa
kinachosadikiwa kuwa ni kuwa na
madeni mengi aliyokuwa akidaiwa na watu mbalimbali.

Jeshi la polisi Wilayani Kilombero
limethibitisha kuwepo kwa taarifa za
mkazi huyo kujinyonga.

Wakati huo huo kijiji hicho cha
Michenga kinataraji kusoma mapato
na matumizi
ya kijiji mwishoni mwa wiki hii kwa
muujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hocho Bwana
Idi Kamila.

Bwana Kamila ameuambia mtandaao
huu kuwa vikao vya ndani
vitakapokamilika
hiii leo taarifa itawekwa hadharani
siku ya kusoma mapato na matumizi
hayo.

KINANA KUONGEA NA WAKAZI WA IFAKARA KESHO

Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi Taifa Bwana
Abdurahaman Kinana kesho
anataji kufanya ziara ya siku moja
Wilayani Kilombero na kuzungumza
na
Wananchi katika eneo la stendi ya
Kwa Makali.

Katibu wa siasa na uenezi CCM
Wilaya ya Kilombero Bwana
Pellegrine Kifyoga
ameiambia Habarikwanza kuwa
lengo la ziara hiyo ni
kuhamasisha ,kuangalia
utekelezaji wa ilani ya chama hicho
na kukagua uhai wa chama na
jumuiya
zake.

Bwana Kifyoga amesema kuwa
Bwana Kinana atafungua mashina ya
wakereketwa
na miradi ya kijamii na baada ya
hapo atazungumza na wananchi
pamoja na
wanachama wa CCM katika mkutano
wa hadhara utakaofanyika saa tisa
alasiri
katika Eneo la Stendi ya Kwa makali
Ifakara Mjini.

Katika Ziara ya Katibu huyo wa CCM
atambatana na Viongozi wa CCM
TAIFA, Katibu
wa NEC Itikadi na uenezi Bwana
Nape Nnauye na Katibu wa Nec
Oganaizesheni
Taifa Bwana Mohamed Seif  Khatib.

Amewataka wanachama na wananchi
kwa ujumla kujitokeza kwa wingi
kuwasikiliza
viongozi hao na kupokea maelekezo
yatakayotolewa na viongozi hao
katika
mkutano huo ili waweze kuyafanyia
kazi zaidi

Friday, April 5, 2013

SHILINGI BILIONI 3.3 KUTUMIKA KATIKA MLADI WA UMWAGILIAJI KILOMBERO

SHILINGI BILIONI 3.3 KUTUMIKA KATIKA MLADI WA UMWAGILIAJI KILOMBERO .

JUMLA ya Fedha shilingi Bilioni 3 Milioni 396 na Laki 9 na Elfu 9 Mia 2 na Tano zitatumika kama Gharama ya Ujenzi wa  Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa Wilayani Kilombero.

Kwa muujibu wa Taarifa ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero juu ya Mradi wa Ujenzi wa  Banio na Mfereji wa Umwagiliaji imeeleza  kuwa fedha zilizopatikana mpaka sasa ni Milioni 510 Laki 2 na Elfu 61 Mia 3 na Sabini na Tano Huku fedha zinazohitajika kukamilisha Ujenzi wa Skimu zikiwa ni Bilioni 2 milioni mia 916 Laki 6 na Elfu Arobaini na Saba Mia 8 na Thelathini na Tatu.

Taarifa imefafanua kuwa kati ya fedha hizo shilingi Milioni 416 na Laki 4 Elfu Sitini na Saba na Mia 3 Sabini na moja zimetumika katika Ujenzi wa Miundombinu Mfereji Mkuu Mita 900, Mifereji ya Kati 3 Mita 925 na Maumbo mbalimbali 12.

 Sehemu ya ujenzi wa mladi wa umwagiliaji wilayani kilombero  
(picha na Henry Bernard Mwakifuna.)
Mradi huo utakaosaidia upatikanaji wa uhakika wa Chakula na ongezeko la Kipato kuondokana na Kilimo cha kutegemea Mvua utasaidia Kaya 1204.

Mradi huo wenye eneo la Ukubwa wa Hekta 675 umepitia hatua mbalimbali tangu  Mwaka 1975 ukiwa chini ya Wachina walioanzisha Kituo cha Mafunzo ya kilimo ukipitia hatua mbalimbali unataraji kukabidhiwa Mwishoni mwa Mwezi ujao.