Sunday, February 23, 2014

AJALI MBAYA YA MOTO YATOKEA MIKESE MKOANI MOROGORO LEO ASUBUHI.

 



 Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka
Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto huo

  Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana  na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Peter Laurence

Friday, February 21, 2014

RT WAWASILISHA MAJINA 40 YA WANARIADHA KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE.

Shirikisho la Riadha Tanzania limewasilisha majina 40 ya wanariadha na sita ya walimu kwenye ofisi ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa tayari kwa ajili ya timu ya taifa ya riadha  kushiriki katika  mafunzo  nje ya nchi.

Rais wa shirikisho la riadha Tanzania Anthony Mtaka amesema wameamua kuwasilisha majina hayo mara baada ya wizara hiyo  kuchukua jukumu la kuwapeleka wanariadha hao nje ya nchi kwenda kujifunza ili baadaye waiwakilishe vema nchi katika mashindano ya Kimataifa.

Wednesday, February 19, 2014

WADAU MBALIMBALI WAHIMIZWA KUENDELEA KUTOA MISAADA KUWASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MKOANI MOROGORO.


Serikali Mkoani Morogoro imefanikiwa kujenga mahema 330 katika vijiji viwili vilivyoathirika na Mafuriko katika wilaya ya Kilosa na Mvomero, ambavyo ni Magore na Mateteni, huku lengo la serikali likihitaji kujenga mahema 520 ili kumuwezesha kila wananchi kuwa na sehemu yake ya kuishi.

Friday, February 14, 2014

KIVUMBI CHA LIGI DARAJA LA KWANZA KUENDELEA KUTIMKA KESHO KATIKA VIWANJA TOFAUTI NCHINI


( PICHA BY PETER LAURENCE )
                                            
Timu ya polisi Morogoro imeondoka jana kuelekea Iringa ikiwa tayari kwa mchezo wa ligi daraja la kwanza  dhidi ya LIPULI ya mkoani humo,  mchezo utakaochezwa jumamosi ya Februari 15 katika uwanja wa Samora Iringa.

MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA YA KILOSA AMETAKIWA KUWAITA WALIMU ILI KUWAELEZA UKWELI WA MATATIZO YAO.


Mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya wilaya ya kilosa masalu mayaya,ametakiwa kuwaita walimu wote wa wilaya ya kilosa ili kuweza kuwaeleza matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.

Wito huo umetolewa Februari 13 mwaka huu na mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya kilosa mheshimiwa Amer Mubarak katika kikao cha kamfed kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo wakati kamfed ilipokuwa ikikabidhi vitabu vya wanafunzi wa sekondari .
Mubarak emesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kujua matatizoyanayowakabili na kuyatafutia ufumbuzi,lengo likiwa ni kuongeza ufaulu mashuleni.
Pia amezitaka bodi za shule kuwa makini nakupa ulewa  wa matatizo yashule zao na kujaribu kutatua na ikishindikana wafike wilayanikuomba nsaada.
;
Aidha mwenyekiti wa halmashuri hiyo ametaka wananchi wahamasishwe kujenga nyumba za walimu karibu na shule ili kuwapa wepesi katika kufanya kazi yao ya kufundisha.

WILAYA YA KILOSA NA WILAYA MPYA YA GAIRO WAMEPOKEA MSAADA WA VITABU AROBAINI NA SABA ELFU NA THELATHINI


      Jumla ya vitabu arobaini na saba elfu na thelathini February 13 mwaka huu  vimetolewa kwa shule za sekondari  wa kumi na tisa wilayani kilosa na shule sita wilaya mpya ya Gairo.

      Vitabu hivyo vimetolewa na shirika la camfed ambalo linashughulikia kwa kuwasaidia watoto walio mashuleni wasio na uwezo licha ya kutoa vitabu na vifaa vingine mashuleni ,pia shirika hilo hutoa karo za shule na mavazi kwa wanafunzi hao.
        Akikabidhi vitabu hivyo kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilosa Amer  Mbaraka Afisa mradi wa kamfed ambaye pia ni mlezi wa kafed mkoani morogoro Deogratius john amesema kuwa kamfed imedhamilia  Nyanja ya elimu ili kufanikisha mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa  yaani [BRN].
         Kati ya vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Dunia yangu bora,How to read English,English study guide,mathematical study guide na biology studyguide
Pia bwana Deogratius John amewataka walimu kupanga mkakati bora kwa kila mwanafunzi apate vitabu hivyo na kuvitumia ipasavyo.