Wednesday, July 23, 2014

VIJANA ZAIDI 100 WA CHADENA WILAYANI ULANGA WAJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM



 BAADHI YA VIJANA AMBAO NI AWALI WALIKUWA WANACHAMA WA CHADEMA WAKIONYESHA KADI ZAO MPYA ZA  CHAMA CHA MAPINDUZI  CCM


Vijana zaidi ya 100 ambao ni wanachama wa chama cha Demokrasia  na maendeleo  CHADEMA    wilaya ya Ulanga  mkoani Morogoro wamekihama chama hicho  na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).
Pamoja na vijana hao pia Viongozi wa juu wa chama hicho wilayani humo  wakiwemo Mwenyekiti wa wazee wa chadema ambaye  pia ni mjumbe wa halmashauri ya mkoa wa chama hicho ndugu Philipo Zimani na Kaimu mwenyekiti wa chadema jimbo la ulanga mashariki  ambaye pia ni katibu kata wa chadema kata ya ruaha wilayani humo Deodatus Charleswamekihama chama hicho na kujiunga na CCM.
MRATIBU WA WAZEE WA CHADEMA NDUGU ZIMANI  NA  KATIBU KATA WA CHAMA HICHO WILAYANI HUMO DEODATUS CHARLIES, WAKIKABIDHI BENDERA ZA CHAMA HICHO KWA UONGOZI WA CCM.
 
Hatua hiyo ya wanachama hao wa CHADEMA kujiunga na CCM imekuja kufauatia maendeleo mbalimbali yanatekelezwa na mbunge wa jimbo hilo la Ulanga Mashariki Serina Kombani, Kama vile ujenzi wa Barabara na ujenzi wa Soko.
Baadhi ya viongozi wa CCM na wale kutoka chama cha CHADEMA waliokiama chama hicho na kujiunga na CCM
Uwajibikaji wa viongozi wa serikali katika majukumu yao wilayani humo ni moja ya sababu inayowafanya wanachama wa vyama vya  upinzani kurudi chama cha mapinduzi  CCM.

WAZAZI NA WALEZI WANUFAIKA NA SHIRIKA LA HUDESA KATIKA KUPUNGUZA UDUMAVU WA WATOTO NA VIFO VYA KINAMAMA



Shirika lisilokuwa la kiserikali HUDESA linalofadhiliwa na USAID Kwa ushirikiano na AFRICARE linaendesha mafunzo ya lishe bora kwa kina mama wajawazito na wanaonyonyesha kwa lengo la kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka miwili wilayani kilosa mkoani morogoro. 


                           Afisa mradi ustawi wa HUDESA wilayani kilosa Hawa Hatibu

                                   Viazi lishe kwa ajili ya watoto na kinamama wanaonyonyesha

Akizungumzia malengo ya HUDESA julai 22 mwaka huu Afisa ustawi wa shirika hilo wilayani kilosa Hawa Hatibu amefafanua kuwa mwanzo bora ni siku elfu moja akiwa na maana toka motto yupo tumboni hadi kuzaliwa kwake na kufikia umri wa miaka miwili [2]ameeleza kuwa kitaalamu motto anapokosa lishe bora kwa kipindi hicho anaweza kudumaa kiakili na kimwili.
                                                          Bustani ya kiroba

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa katika mpango huo wa mwanzo bora wanafundisha kinamama jinsi ya kuandaa chakula bora kwa mtoto sambamba na hapo wameandaa bustani ya mbogamboga za majani pamoja na viazi lishe ambavyo hutumika kumuandalia chakula mtoto.
                                     Baadhi ya walezi wakiwa kwenye bustani
Kwa upande wake Salehe kaombwe ambaye na mhudumu wa afya wa majumbani kata ya kasiki wilayani kilosa amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuepukana na vifo vya kinamama na udumavu wa watoto.
                                              Bustani ya mbogamboga aina ya chainizi

Nao baadhi ya kinamama wa wilayani kilosa mkoani morogoro Husna Rashidi na Amina bint Ally wamesema kuwa wanalishukuru sana shirika la HUDESA kwa kuwapatia elimu ya mafunzo ya jinsi ya kuwaandalia lishe iliyobora watoto wao ili waweze kukua vizuri na kuweza kuepukana na magonjwa yanayoepukika.



Friday, July 18, 2014

HAWA GHASIA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Mheshimiwa Hawa Ghasia amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa kusimamia vizuri vyanzo vya mapato vilivyopo Wilayani humo  ili kuleta maendeleo na kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili. 
     waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI)Hawa Ghasia     akifungua barabara ya lami inayoelekea ofisi za halmashauri ya wilaya ya kilosa

Ghasia amesema hayo Julai 18 mwaka huu  alipokuwa kwenye mkutano maalumu na watumishi pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo kwenye ziara yake  ya siku moja  wilaya ya kilosa yenye lengo la kukagua na kuzindua miradi mbambali ya maendeleo wilaya ya kilosa mkoani morogoro.
            Baadhi ya wananchi waliohudhulia katika ufunguzi wa barabara ya lami inayoelekea  ofisi za halmashauri ya wilaya ya kilosa

Ghasia amesema kuwa endapo vyanzo vya mapato vitasimamiwa vyema Halmashauri itakuwa na uhakika wa kupata mapato ya kutosha ambayo yataweza kusaidia kununua magari kwa ajili ya matumizi ya maendeleo kwa Halmashauri na mahitaji mengine pia kuhakikisha inatatua changamoto ya uwepo wa Makaimu Wakuu wa Idara kwa kuteua Watendaji wenye sifa ili kuwa na uadilifu katika shughuli za kiutendaji.
              Maafisa usalama nao hawakuwa nyuma kuhakikisha shughuli zote zinakamilika kwa amani

Sambamba na hayo katika ziara yake ya siku moja Wilayani Kilosa Ghasia amepata wasaha wa kuzindua Barabara ya lami Bomani na Hospitali ya Wilaya,Mradi wa wodi ya wagonjwa grade two na ukarabati wa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Wilaya,Mradi wa Kilimo Shadidi na kupokea taarifa ya mradi wa upimaji viwanja vya wahanga wa mafuriko Tarafa ya Magole pia amewasisitiza Madiwani na Watendaji wa Halmashauri kusimamia mapato na kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata taratibu zote za kazi.

Saturday, July 12, 2014

WATUMISHI WA AFYA WATAYEBAINIKA KUWAUZIA WAGONJWA DAMU KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA

















Jamii imetakiwa kuwa na ushirikiano na wahamasishaji  wa damu salama ili kuwabaini  na kuwachukulia hatua kali za kisheria watumishi wa afya watakaobainika kutumia vibaya damu inayotolewa na wananchi kwa kuwauzia wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

Hayo yamebainishwa mkoani morogorogo katika mafunzo ya uhamasishaji wa mpango wa taifa wa kuchangia damu salama na Afisa uhamasishaji Bernadino Medaa, na kusema kuwa  suala la uuzaji wa damu sio suala la kupambana na  mpango wa Damu Salama pekee bali la wananchi wote kwa pamoja kushirikiana  kulitokemeza kabisa jambo la uuzaji wa damu wagonjwa wanaohitaji.

Ili kutokomeza tabia hiyo, Afisa  Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Damu salama, nchini Bernadino Medaa ameitaka jamii kuwa na ushirikiano na shirika la Damu salama ili kuweza kuwadhibiti waharifu hao ambao ni watumishi wa afya wanauza damu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.















Kwa upande wake Afisa  mahusiano wa mpango wa taifa wa damu salama, Rajabu Mwenda amewataka watumishi hao wa afya kuacha mara moja tabia ya kuwauzia wagonjwa wanaohitaji huduma ya Damu, kwani kufanya hivyo kunakatisha tama a kwa wananchi kushindwa kuijitokeza kuchangia huduma hiyo ya Damu.

Baadhi ya wahamasishaji wakiwa makini katika mafunzo hayo














 \
















Nao Washiriki wa mafunzo hayo Lacas Michael, Afisa uhamasishaji kanda ya Mashariki na na Evelyne Kussaga, afisa masoko wa Mpango wa Taifa wsa Damu salama, wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa wa ukusanyaji wa damu salama  hasa mashuleni ambao wanafunzi ndio wadau wakubwa wa ukusanyaji damu nchini .

Mafunzo hayo yamedumu kwa muda wa siku sita ambayo yameanza tarehe 6 mpaka tarehe 12 mwezi huu, ukiwakutanisha wahamasishaji wa damu salama na watumishi wa afya kote walipo nchi kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya umasishaji wa utoaji wa damu salama kwa wananchi.

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA SABA AFICHWA NDANI KUTOKANA NA KUWA NA ULEMAVU WILAYANI KILOSA



Mtoto anayefahamika kwa jina la Devota Dalule mwenye umri wa miaka saba (7)  mkazi wa Dumila Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro amefungiwa ndani  kwa muda wa miaka saba na Mama yake mzazi anayetambulika kwa jina la Sarah Mazengo mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Dumila Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kutokana na mtoto huyo kuwa na ulemavu wa miguu .
                                         Mtoto Devota Dalule akiwa hopspitali ya wilaya ya kilosa

Kwa mujibu wa Daktari Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kilosa Shedrack Mponzi amesema mtoto  huyo amefika hospitalini hapo  usiku wa kuamkia julai 12 mwaka huu akiwa  tatizo la Utapiamlo na kusema kuwa hali yake bado haijatengemaa na leo hii amepewa rufaa ya kwenda hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.

                                  MtotoDevota Daluleakiwa hospitali ya wilaya kilosa akiendelea kupatiwa matibabu

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Kilosa Saidi Kataluma amesema kuwa matatizo haya ya utesaji na unyanyasaji wa watoto kwa wilaya ya Kilosa tatizo hilo ni la pili la kwanza limetokea julai 3 mwaka huu lililomuhusisha mtoto aliyefahamika kwa jina la Selemani Salumu mwenye umri wa miaka mitatu (3) ambaye ametelekezwa na mama yake mzazi Mwamini Juma mwenye umri wa miaka 20 kutokana na mtoto huyo kuwa na kichwa kikubwa. Na tukio la pili ni hili la mtoto Devota Dalule ambapo inasemekana mtoto huyo amewekwa ndani kwa kipindi chote cha miaka saba na kutopata huduma muhimu kama chakula pamoja na mavazi na inasemekana kuwa mama huyo humficha mtoto huyo uvunguni ili asionekane kwa watu kutokana mtoto huyo kuwa na ulemavu.
                                     muuguzi wa hospitali ya wilaya kilosa akimuhudumia mtoto Devota Dalule


Kataluma amewataka wananchi kuendelea kufichuwa maovu yote yanayotendeka katika jamii kwa ajili ya kutokomeza matatizo hayo ya ukatili dhidi ya watoto wadogo.
Kwa upande wao wananchi wa Wilayani  Kilosa Lameck Mkude na Jane Amandus wamesema kuwa vitendo hivi vinahathiri sana ukuaji wa mtoto na wameviomba vyombo vya sheria pamoja na wananchi kusimamia mambo haya kwa ajili ya kuweza kuyatokomeza na wameongeza kuwa mtoto hata kama atakuwa na ulemavu ana haki ya kuishi kama mtoto asiye na ulemavu.

Friday, July 11, 2014

DAKTARI FEKI AKAMATWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO




Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Renard Paul
Polisi mkoani morogoro inamshikilia Karume Kauzu Habibu Mkazi wa Riti kwa kujifanya daktari katika haspitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro ambapo  amekuwa akioneka maeneo hayo huku akiwa mevalia mavazi ya udaktari. 

Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi Renard Paulo amethibitishwa kutokea kwa tukio hilo na amesema mtuhumiwa  huyo baada ya kukaguliwa amekutwa na vitambulisho vinne tofauti huku kingine kikionyesha anajiandaa kurudia mtihani wa kidato cha nne, makazi yake yakiti RITI mkoani Morogoro na huku kitambulisho chake kimoja kinaonyesha kuwa alikuwa anasoma Kigoma. 
Daktari feki aliyevaa koti jeupe Karume Kauzu Habibu akiwa chini ya ulinzi
Baadhi ya Vitambulisho vya daktari huyo feki.































  Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji Francis Semwene amesema alipata taarifa toka kwa muuguzi wa zamu na kuweka mtego ulifanikisha kukamatwa kwa daktari huyo feki.

Matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini kwa baadhi ya watu wasio waaminifu kujiingizia vipato kwa njia zisizo halali na kutishia usalama na afya za wananchi.

Waandishi wa Habari nao Hawakuwa nyuma

Wednesday, July 9, 2014

WAKULIMA WILAYANI KILOSA WANUFAIKA NA MKUHUMI


Afisa Elimu kutoka shirika la mkuhumi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Shadrack Yoash amewataka wakulima kuacha kulima kilimo cha mazoea na kinachoathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi na badala yake walime kilimo cha kisasa ili waweze kuepukana na umasikini.
Hayo ameyasema julai 8 mwaka huu kwenye sherehe za wakulima wa shamba darasa zilizofanyika katika kijiji cha Lunezi kitongoji cha Manyomvi kata ya Lumuma Wilayani humo ambazo zimeandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali Mkuhumi.
Yoash amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yalivyo na kasi kwa kipindi hiki huku wananchi wakiendelea kulima kilimo cha mazoea hawataweza kupata mavuno ya kutosha na kwamba watazidi kukata misitu kwa ajili ya kuongeza mashamba hali itakayo sababisha kutokea kwa ukame na hatimaye wakulima kuwa na kipato kidogo na kushindwa kumudu familia zao.
Ameongeza kwa kusema kuwa  shirika la Mkuhumi umeanzisha rasmi shamba Darasa tangu Mwaka 2010 katika vijiji 8 Wilaya ya Kilosa na kwamba kila Kijiji  kuna vikundi viwili vinavyotekeleza mradi wa shamba darasa na kwamba wameanzisha mfumo wa kutoa zawadi kwa kila kikundi kinachofanya vizuri na mkulima mmoja mmoja kama motisha ili waweze kufanya vizuri.
Katika sherehe hizo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri wilaya ya Kilosa Amer Mubarak ameweza kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pamoja na kikundi ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Tamasha Mkwechi amezawadiwa fedha taslimu elfu thelathini,Agripina Pweleza elfu 25 na Emili Mgabe shilingi elfu 15 na kikundi kimepata baiskeli aina ya foneksi na shilingi elfu 50.
Aidha akizungumza kwa niaba ya wakulima wa shamba Darasa katika Kitongoji cha Manyomvi Bi Tamasha Pweleza amesema kuwa wanaushukuru mradi wa Mkuhumi kwa kutoa mafunzo hayo na kwamba wananchi   wameweza kufuatilia kwa kina na wameiomba serikali itoe mikopo ya pembejeo kwa wakulima hao ili waweze kuendeleza kilimo.

Monday, July 7, 2014

UKATILI WA KIJINSIA SASA BASII



Shirika la usaidizi wa kisheria mkoano morogoro Paralegal limeendesha mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia julai 5 mwaka huu wilayani kilosa mkoani mkoani morogoro.
Akizungumza katika mdahalo huo Meneja wa shirika hilo mkoani morogoro Flora Masoy amesema kuwa wanatoa mafunzo hayo  kwa wananchi ili waweze kujitambua na kutokomeza  vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vitendo vya ukatili hufanyiwa akina mama pamoja na watoto.

Ameongeza kwa kusema kuwa kinamama wengi hutendewa ukatili wa kijinsia na kubaki kimya kutokana na hofu wanayopewa na wanaume zao na kuwataka kina mama kuacha kukaa kimya kwani nao wanahaki sawa na mwanaume na kukaa kimya kwa mwanamke ni sawa na kujikatili wewe mwenyewe na kuwaomba kina mama na jamii kiujumla kufichua maovu yote ya unyanyasaji wa kijinsia bila kuwa na hofu yoyote.
                                                   Wajumbe wakiwa kwenye mdahalo

Wakizungumza katika mdahalo huo baadhi ya wajumbe katika mdahalo huo Baby Mussa na Stella Venus wamesema kuwa wanalishukuru shirika la Paraleg kwa kutambua maovu yaliyoko kwenye jamii  na kuamua kuhamasisha wananchi kuachana na ukatili wa kijinsia kwa kutumia midahalo hiyo na kuongeza kuwa wanaomba katika mchakato wa kuipata katiba mpya wajumbe waliangalie swala la usawa kati ya mwanamke na mwanaume katika jamii .

Aidha wamesema kuwa waliyoyapata katika mdahalo huo kwenda kuyatendea kazi katika jamii zao wanapotoka na kuhahakikisha kila mtu anapata haki yake kwa kusema kuwa kwa wilaya ya kilosa wanaume wanaume hutelekeza familia kwa mwanamke, mwanamke kuamrishwa kutozaa na mwanamke kukosa haki yake ya kimsingi katika ugawaji wa mirathi na kusema kuwa watasimama imara katika kupatikana kwa haki kwa kila mtu.

                       Mmoja wa wajumbe wakiwa kwenye mdahalo wakijadiliana kuhusu ukatili wa kijinsia


        Wajumbe wakiwa kwenye vikundi kujadiliana kuhusiana na mada ya ukatili wa kijinsia