Mara baada ya baraza la mitihani nchini Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne waliofanya mtihani yao mwezi wa kumi mwaka jana,hali imekuwa ni ya kupishana kwenye migahawa ya mawasiliano kwa wanafuzi na wazazi wa watoto mbali mbali ili kuweza kujua matokeo hayo.
Mara baada ya baraza la mitahani Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne na kuyaweka katika mtandao wa baraza hilo,watahiniwa mbali mbali wamejitokeza katika migahawa ya mawasiliano kuangalia ufaulu wao kwa sehemu mbali mbali nchi.
Mara baada ya baraza la mitihani nchini Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne waliofanya mtihani yao mwezi wa kumi mwaka jana,hali imekuwa ni ya kupishana kwenye migahawa ya mawasiliano kwa wanafuzi na wazazi wa watoto mbali mbali ili kuweza kujua matokeo hayo.
Mtandao huu umefanikiwa kupita katika sehemu mbali mbali za migahawa hiyo ya mawasiliano kwa mji wa Njombe na imekuta idadi kubwa ya wanafunzi waliojitokeza katika kuangalia matokeo hayo yaliyotangazwa na baraza la mitihani hapa nchini.
Hali hii imekuwa ikiwapa wakati mgumu kwa wanafunzi kuweza kupokea matokeo yao mara baada ya kufanya mitihani yao mwezi wa kumi mwaka 2010 na kusubiri matokeo yao kwa kipindi chote cha takribani miezi mitatu.
Akizungumza na mtandao huu mmoja wa wanafuzi waliohitimu mwaka huo wa 2010 katika shule ya mpechi wilayani Njombe mkoani Njombe aliyekataa kutaja jina lake anasema matokeo ya mwaka huu kwa shule za serikali sio mazuri sana kutokana na shule za serikali kubwa na upungufu wa walimu ,vile vile kutokuwepo kwa vifaa vya ufundishaji ikiwemo vifaa vya maabara kwa nyingi za serikali.
Kijana huyu anasema kwa upande wake yeye matokeo yake hayajakuwa mazuri sana kama alivyokuwa akitarajia.
Ameongeza kuwa moja ya vitu ambavyo pia vimepelekea kuanguka kwao katika ufaulu ni pamoja na kitendi cha serikali kuondoa mtihani wa kidato cha pili hali inayopelekea kwa wanafunzi waliofanya vizuri na wasiofanya vizuri kuendelea katika kidato cha tatu hivyo kutowafanya wanafunzi wengi kutokuwa makini hali inayowapelekea kufika kidato cha nne wakiwa bado hawana uwezo mzuri kitaaluma.
Hata hivyo baadhi ya wazazi wilayani hapa wamesema kuwa ufaulu wa watoto wao wengi wao umekuwa si mzuri sana kutokana na watoto wao wengi waliokuwa shule za serikali kutokufanya vizuri kama wale wenzao wa shule za binafsi.
Mtandao huu haukufanikiwa kukutana na afisa elimu wa wilaya hii ya Njombe kuweza kuzungumzia ufaulu kwa wilaya ya Njombe na shule zake kwa ujumla.