SHULE YA SEKONDARI MLABANI WILAYANI KILOMBERO YAKOSA VYOO KWA KIPINDI CHA MIAKA NANE
Shule ya sekondari ya Mlabani iliyopo kata ya Ifakara wilayani Kilombero, inakabiliwa na uhaba wa vyoo kwa muda wa miaka minne sasa na kuwafanya wanafunzi wa shule hiyo kuwa katika hali ya hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
Hayo yameelezwa katika taarifa ya shule hiyo iliyosomwa na makamu mkuu wa shule,hiyo mwalimu Idrissa Lyoko katika mahafali ya kwanza ya shule hiyo kwa mgeni rasmi, imeeleza kuwa shule hiyo ina choo chenye matundu manane tu, ikiwemo matundu sita yanayotumiwa na wanafunzi wa shule hiyo wapatao 635.
Taarifa hiyo imeeleza Kwa sasa shule hiyo inahitaji matundu 28 ya choo
na ina upungufu matundu 22 ya choo.
Risala hiyo imeeleza kati ya wanafunzi hao wavulana 350 na wasichana 285, pia walimu wako kumi, wanaume sita na wanawake wanne, shule ina mchepuo wa sayansi, biashara na sanaa.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambayo ni ya kwanza katika shule hiyo meneja wa shirika la PLAN INTERNATIONAL Tawi la Ifakara, bwana HAIDARI MFINANGA amesema viongozi wa serikali za vitongoji vilivyopo katika vijiji vya Mlabani na Katindiuka na uongozi wa halmashauri wapange mikakati ya kuiendeleza shule hiyo kimajengo
Bwana Mfinanga amesema shirika lake la Plan halitasaidia tena katika ujenzi wa majengo bali kwa sasa inafadhili watoto wanaosoma, hivyo amewataka jamii na wazazi washirikiane kuleta maendeleo ya shule hiyo kwa njia ya michango.