Monday, December 8, 2014

WANANCHI WA WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO WATAKIWA KUWA MAKINI KWA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA KIJIJI KWA KUCHAGUA KIONGOZI ATAKAYEJALI MASLAHI YA WANANCHI



Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo amewataka wananchi wa wilayani kilosa kuwa makini kwa kipindi hiki cha kampeni kwa kuwachagua viongozi watakaojali maslahi yao. 
                                   Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo akiwa ofisini kwake.

Ameyasema hayo December 8 mwaka huu wakati akizungumza na HABARIKWANZA  ofisini kwake kuhusiana na hali ya kampeni inavyoendelea wilayani kilosa na ameeleza kuwa hali ya kampeni inaendelea vizuri na kwa amani.
Mh:Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo akiwa anaongea na HABARIKWANZA ofisini kwake

Aidha amewataka viongozi wanaofanya kampeni kutumia lugha nzuri zisizo za matusi kwani siasi haiendeshwi kwa matusi na amesema kuwa mwanasiasa anayetumia lugha chafu za matusi huyo hajakomaa kisiasa na hana sera ya kuwaambia wananchi ili wamchague.

Pia Tarimo amewataka wananchi kusoma katiba mpya ambayo inatakiwa kupigiwa kura na amewataka wananchi kuwa makini pindi zitakaposambazwa kwa kuweza kuipigia kura pasipo kushawishiwa na mtu au kikundi cha watu kitu  ambacho kitamfanya mwananchi kuipigia kura pasipo ridhaa yake (kushawishiwa) na amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuipigia kura katiba hiyo pindi muda wake utakapofika.