Saturday, April 22, 2017

WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA MBWADE WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO WAILALAMIKIA SERIKALI KWA KUTOKUWA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA KIJIJI

Wakazi wa kijiji cha mbwade wilayani kilosa mkoani morogoro wailalamikia serikali kwa kutokuwa na wenyeviti wa vitongoji na kusababisha kushuka kwa maendeleo katika kijiji Chao kwa kukosa wawakilishi katika vikao vya halmashauri ya kijiji.
Mmoja kati ya wakazi hao aliyeomba jina lake Lihifadhiwe amesema kuwa chanzo cha kijiji hicho kutokuwa na wenyeviti wa vitongoji nikutokana uchaguzi wa mwaka 2014 wa ngazi ya serikali ya mitaa kudai kuwa kuvamiwa nawatu ambao si wakazi wa kijiji hicho ambao walipiga kura jambo ambalo liliwafanya wakazi wa eneo hilo kugomea uchaguzi kutokana na watu hao kuonekana kupiga kura kuchagua mgombea kwa maslahi yao binafsi.

Kwa upande wake kaimu mtendaji wa kijiji hicho Huruma Kandili amesema kijiji hicho kina jumla ya vitongoji vitano ambavyo ni madoto lunch, mkwajuni, kichangani, usagarani, na mtapenda kati ya vitongoji vyote vitano kimoja kina mwenyekiti wa kitongoji ambacho ni kitongoji cha madoto lunch kwa upande wake amesema kuwa kijiji chake hakina wenyeviti wa vitongoji nikutokana na wanakijiji kuvunja masanduku yakupigia kura wakidai kuwa Kuna watu waliovamia uchaguzi ambao si wakazi wa kijiji hicho jambo ambalo amelikanusha na ameeleza kuwa watu hao ni wakazi wa kijiji hicho ila kijiji hicho kina jamii mbili ya wakulima na wafugaji hivyo jamii ya wafugaji watu wakuhama hama wakitafuta malisho yamifugo yao hivyo Muda wa uchaguzi walirudi kwa ajili yakufanya uchaguzi katika kijiji Chao.

Alipotafutwa mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya kilosa Kesi Juma Mkambala kuelezea ukweli wa taarifa hii amesema kuwa yeye hana taarifa kuhusiana na tatizo hilo na ameahidi kulifuatilia.

Thursday, April 20, 2017

KAYA 151 ZIMEATHILIWA NA MAFURIKO KATIKA KATA YA MVUMI WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO

Kaya takribani 151 zimeathilika na mafuriko katika kata mvumi wilayani kilosa mkoani morogoro mafuriko yaliyotokea alfajili ya april 20 mwaka huu na kuathili vitongoji viwili bomba kumi na mvumi A katika kata hiyo.
Akizungumzia hali halisi ya mafuriko hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilosa Kesi Juma Mkambala amesema mafuriko hayo yameathili kaya 151 na kati ya kaya hizo kaya 15 zimebomoka kabisa na wakazi kukosa mahali pa kuishi pamoja na taasisi mbili za serikali ikiwemo shule ya msingi mvumi A pamoja na ofisi ya kijiji kuvamiwa na mafuriko hayo.Ameongeza kwa kusema kuwa tayari serikali imetenga eneo kwa waathilika wa mafuriko hayo kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwapatia chakula huku kamati ya maafa ya wilaya ikiendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Akielezea chanzo cha mafuriko hayo mtendaji kata wa kata ya mvumi Aloyce izdoli amesema kuwa chanzo cha mafuriko hayo ni mto kisangata kujaa maji na kupasua na kuingia katika makazi ya watu na maji kukosa mahali pakutokea kutokana na eneo hilo kutokuwa na kalavati la kupitisha maji kwa kuwa eneo hilo kuna barabara ya lami itokayo dumila kuelekea kilosa hivyo maji kushindwa kupita kwenda upande wa pili wa barabara.

Baadhi ya wahanga wa mafuriko hayo Betha Magesa na Mashaka Rock wamesema kuwa athali walizozipata ni kubwa kutokana na mafuriko hayo kuingia ghafla na wao hawakuweza kuokoa vitu vyovyote katika makazi yao na baadhi yao kukosa mahali pakuishi kutokana na nyumba kubomoka na mazao kuingia maji.

Wednesday, April 19, 2017

BREAKING NEWS MAFURIKO YAWAVAMIA WAKAZI WA MVUMI WILAYANI KILOSA

Wakazi wa mvumi wilayani kilosa mkoani Morogoro waathirika na mafuriko yaliyotokea leo asubuhi na shughuli za uokoaji zinaendelea

Thursday, April 13, 2017

SIMBA YAIBUKA KIDEDEA KATIKA RUFAA YAO DHIDI YA KAGERA SUGAR

Simba wameshinda rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar na wamepewa point tatu baada ya kuibainika mchezaji wa kagera Sugar Mohammed Fakhi alicheza mechi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano katika michezo dhidi ya Mbeya City, Majimaji, African Lyon hizo ndio mechi ambazo amepata kadi za njano
Hivyo simba inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa na point 61 ikifuatiwa na waasimu wao yanga wakiwa na point 56

RUFAA YA SIMBA KUJULIKANA LEO

HATIMA ya rufaa iliyokatwa na Klabu ya Simba dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilimchezesha beki wake Mohammed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, inatarajiwa kujulikana leo baada ya kikao cha Kamati ya Saa 72 ya Usimamizi wa Ligi Kuu itakapokutana. 

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara namba 194, iliyofanyika Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-1. 

Taarifa kutoka kwa kiongozi mmoja wa bodi ya ligi (jina tunalihifadhi) ilieleza jana kuwa, kikao hicho kitafanyika leo kama ilivyopangwa na uamuzi juu ya rufaa hiyo utatolewa baada ya kikao hicho kumalizika. 

'Kikao kipo kama ilivyoelezwa, tayari maandalizi na nyaraka muhimu ambazo zilihitajika zimeshawasili, wajumbe wote wanaohusika wameshataarifiwa juu ya kuhudhuria kikao hicho," alisema kiongozi huyo wa bodi ya ligi. 

Kiongozi huyo alisema kuwa mbali na rufaa hiyo ya Simba, pia kikao hicho kitajadili taarifa za mechi nyingine mbili za ligi hiyo zilizofanyika juzi kwenye viwanja viwili tofauti hapa nchini. 

"Kikao kitajadili pia taarifa za mechi za juzi (Jumatatu) kati ya Mbao FC dhidi ya Simba na mchezo wa Mtibwa Sugar dhidi ya Azam FC, si unajua lazima nazo zijadiliwe kabisa kwa sababu tayari taarifa zimeshatumwa," aliongeza kiongozi huyo. 

Mechi ambazo Fakhi anadaiwa alionyeshwa kadi za njano ni ile iliyofanyika Desemba 17, 2016 katika mchezo namba 122 kati ya Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na nyingine ilikuwa ni Januari 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba, walipokipiga dhidi ya African Lyon ya Dar es Salaam. 

Machi 4, mwaka huu Fakhi alionyeshwa kadi nyingine ya tatu katika mchezo namba 190 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Kagera ilipoikaribisha Majimaji ya Songea. 

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alikaririwa na vyombo vya habari kuwa mchezaji huyo alikuwa na kadi mbili za njano na si tatu kama Simba wanavyodai.