Wednesday, December 18, 2013

Anusurika kuuawa na majambazi wilayani kilosa

Mkazi wa manispaa ya wilaya ya kilosa mkoani morogoro,costa mwamba amenusurika kuuawa baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wanaosadikiwa ni majambazi.


Akizungumzia tukio hilo mtendaji wa kijiji cha munisagara Donald mgulambwa amesema kuwa tukio hilo limetokea dec 17 mwaka huu majira ya saa nane usiku ambapo watu hao walifika nyumbani kwa bwana mwamba na kuvunja mrango kwa jiwe maarufu kama jiwe Fatuma.,
Amesema kuwa majambazi hao ambao wanasadikiwa kuwa ni wane baada ya kufanikiwa kuvunja mlango huo waliingia ndani na ndipo walipoanza kumcharanga kwa mapanga bwana mwamba pamoja na mkewe Chiku Salumu na kasha kufanikiwa kuchukua kiasi cha pesa shilingi laki nane.

Mgulambwa amesema kuwa baada ya majambazi kufanya uhalifu huo majeruhi hao walipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani ndipo majambazi hao wakatokomea kusiko julikana.

Majirani wa eneo hilo walimkimbiza bwana Mwamba katika hospitari ya wilaya ya kilosa kutokana na majeruhi makubwa aliyoyapata huku mkewe akipelekwa katika katika zahanati ya kijiji hicho.

Tukio kama hili ni la pili kutokea katika kijiji cha munisagara ambapo viongozi wa kijiji viongozi wametoa taarifa katika kituo cha polisi wilani kilosa kwa uchungzi zaidi.

Thursday, December 12, 2013

VIKUNDI VYA POLISI JAMII VYAPEWA VITAMBULISHO WILAYANI KILOSA


Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya kilosa peter nsato [SP]Dec 12 ametoa vitambulisho kwa vikundi vya polisi jamii wilayani kilosa.

 Mgeni rasmi SP Peter Nsato akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa vikundi vya polisi jamii Wilayani Kilosa.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya kilosa peter nsato [SP] amevitaka vikundi vya polisi jamii wilayani humo kutenda kazi kwa uadilifu na kuwataka kufichua uhalifu punde unapotokea,Pia katika kuwapatia vitambulisho  wanavikundi hao wamepewa mavazi ya kujitambulisha kuwa askari [reflector]pindi wawapo kazini.
 Matanda Ally matanda akipokea mavazi ya polisi jamii kutoka kwa SP Peter Nsato mara baada ya kupokea kitambulisho

 Aidha mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya kilosa [ASP]Antony mkwawa amesema kuwa jeshi la polisi limeamua kuanzisha uhamasishaji wa polisi jamii na ulinzi shilikishi lengo likiwa ni kupungunza uhalifu unaotokea katika jamii na kulinda mali za wananchi,Na kuongeza kuwa jeshi la polisi linauhaba wa polisi na kuwataka wananchi kushirikiana vizuri na polisi jamii hao ili kumaliza kabisa matukio ya kiharifu yanayotokea katika jamii.            
 
       
 Aliyesimama ni mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya kilosa ASP Antony mkwawa na wapili Kushoto kwake ni SP  Peter Nsato.

Aidha katika risala iliyoandaliwa katika vikundi hivyo ambavyo ni UKOMBOZI ULINZI SHIRIKISHI Kutoka kata ya kasiki,MALIWASO ULINZI SHIRIKISHI kata ya mbumi na MTENDENI B ULINZI SHIRIKISHI,Wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuwashirikisha wanajamii kwani imesaidia kuvumbua matatizo yaliyopo kwenye jamii.
                 Hata hivyo wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi kama vile tochi,usafiri,makoti kwa ajili ya mvua na kuliomba jeshi la polisi tarafa ya kilosa liendelee kuwahamasisha wadau mbalimbali katika maeneo yao kuvisaidia vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi.