Thursday, December 12, 2013

VIKUNDI VYA POLISI JAMII VYAPEWA VITAMBULISHO WILAYANI KILOSA


Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya kilosa peter nsato [SP]Dec 12 ametoa vitambulisho kwa vikundi vya polisi jamii wilayani kilosa.

 Mgeni rasmi SP Peter Nsato akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa vikundi vya polisi jamii Wilayani Kilosa.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya kilosa peter nsato [SP] amevitaka vikundi vya polisi jamii wilayani humo kutenda kazi kwa uadilifu na kuwataka kufichua uhalifu punde unapotokea,Pia katika kuwapatia vitambulisho  wanavikundi hao wamepewa mavazi ya kujitambulisha kuwa askari [reflector]pindi wawapo kazini.
 Matanda Ally matanda akipokea mavazi ya polisi jamii kutoka kwa SP Peter Nsato mara baada ya kupokea kitambulisho

 Aidha mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya kilosa [ASP]Antony mkwawa amesema kuwa jeshi la polisi limeamua kuanzisha uhamasishaji wa polisi jamii na ulinzi shilikishi lengo likiwa ni kupungunza uhalifu unaotokea katika jamii na kulinda mali za wananchi,Na kuongeza kuwa jeshi la polisi linauhaba wa polisi na kuwataka wananchi kushirikiana vizuri na polisi jamii hao ili kumaliza kabisa matukio ya kiharifu yanayotokea katika jamii.            
 
       
 Aliyesimama ni mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya kilosa ASP Antony mkwawa na wapili Kushoto kwake ni SP  Peter Nsato.

Aidha katika risala iliyoandaliwa katika vikundi hivyo ambavyo ni UKOMBOZI ULINZI SHIRIKISHI Kutoka kata ya kasiki,MALIWASO ULINZI SHIRIKISHI kata ya mbumi na MTENDENI B ULINZI SHIRIKISHI,Wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuwashirikisha wanajamii kwani imesaidia kuvumbua matatizo yaliyopo kwenye jamii.
                 Hata hivyo wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi kama vile tochi,usafiri,makoti kwa ajili ya mvua na kuliomba jeshi la polisi tarafa ya kilosa liendelee kuwahamasisha wadau mbalimbali katika maeneo yao kuvisaidia vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi.

No comments:

Post a Comment