Viongozi wa vijiji na kata wametakiwa kusimamia kwa juhudi
ujenzi wa maabara tatu za sayansi katika shule za sekondari.
Katibu mkuu wa mkoa wa morogoro aliyevaa suti ya kijivu Elias Ntandu akitoa maelekezo ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari kutukutuakiwa pamoja na viongozi alioambatana nao katika ziara ya ujenzi wa maabara.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala mkoa wa morogoro Elias
Ntandu mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa ziara yake ya kutembelea shule 39 za
sekondari katika wilaya ya kilosa ambapo amekagua ujenzi wa maabara katika
shule hizo na kujionea hali halisi ambapo amesema kuwa shule nyingi za sekondari
Viongozi wakiwa wanakagua maabara katika shule ya sekondari Mazinyungu iliyopo wilayani kilosa
hazijakamilisha ujenzi huo wa
maabara ambalo ni tamko la mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa hadi kufikia mwezi wa kumi na moja 2014 maabara
hizo
Maabara ya Fizikia ambayo inatumika ya shule ya sekondari Mazinyungu iliyopo wilayani kilosa mkoani morogoro.
zinatakiwa kukamilika na kwa viongozi wa kijiji na kata wanatakiwa
kukamilisha ujenzi huo mapema ya mwezi wa kumi 2014.
Diwani wa kata ya Mbumi Mama mbaruku akitoa maelekezo kwa viongozi kuhusu ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Mbumi iliyopo katika eneo lake la kiutawala.
Katika ziara hiyo ya kukagua ujenzi wa maabara iliyoambatana
na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya kilosa Elias Tarimo,Katibu
tawala wilaya Hilary Sagala Afisa mipango wilaya Lwidin Ngakoka
Baadhi ya viongozi wakiwa katika shule shule ya sekondari Mvumi kabla ya kwenda kukagua ujenzi wa maabara.
Afisa elimu
sekondari wilayani kilosa Jonas Ntigoza pamoja na Afisa elimu Taaluma mkoa Raphael
Pagala na
viongozi wengine kutoka wilayani kilosa ambapo Mkuu wa wilaya ya
kilosa Elias Tarimo amewataka
Katibu Tawala mkoa wa Morogoro Elias Ntandu akiwa na mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo wakiwa wanajumuika katika kuchimba shimo ambalo litatumika pindi maabara itakapokuwa tayari.
viongozi kupiga mahesabu vizuri kughusu ujenzi
huo wa maabara ili pindi wanapotoa gharama ya uchangiaji kwa kila mwananchi
kusiwe na utata kwani ujenzi wa maabara
unategemea nguvu ya wananchi.
Afisa elimu sekondari Jonas Ntigonza akiwa anaangalia ujenziwa maabara katika shule ya sekondari Gongwe iliyopo mvumi wilayani kilosa.
Aidha Tarimo amewataka viongozi wa kisiasa kuacha kuingilia
shughuli za ujenzi wa maabara kisiasa kwani
Maabara ya shule ya sekondari Ludewa iliyokuwa hatua za mwisho za umaliziaji.
jambo hilo la ujenzi si swala la
kisiasa na kuwataka wananchi kujitoa kwa hali na mali ili kukamilisha ujenzi
huo wa maabara kwa kila shule ya sekondari mapema ya mwezi wa kumi 2014.
Ujenzi wa maabara ukiwa katika ngazi ya uchimbaji wa msingi katika shule ya sekondari Mkulo Iliyopo wilayani kilosa mkoani Morogoro na viongozi wakiwa wanakagua ujenzi huo.
Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo akiwa katika uwajibikaji kwa vitendo kwa kuchimba msingi katika shule ya sekondari Kutukutu.