Monday, October 27, 2014

UJENZI WA MAABARA WAPAMBA MOTO



Diwani wa kata ya Ulaya Wilayani kilosa mkoani Morogoro Raimond Chengula amewataka wananchi kuendelea kuchangia ujenzi  wa maabara katika shule ya sekondari Ukwiva.
Wakwanza kushoto ni Diwani wa kata ya Ulaya Raimond Chengula wakatikati ni Afisa mifugo kijiji cha Mhenda piua ni mhasibu wa ujenzi wa maabara na wa mwisho ni Katibu Tarafa wa Tarafa ya Ulaya Raphael Mvurungu.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wananchi walipokuwa wanasomewa mapato na matumizi kuhusu ujenzi wa maabara ambao kwa sasa umefikia hatua ya msingi ambapo Mhasibu wa kamati ya ujenzi Juma Khassim amewasomea mapato na matumizi ya michango waliyoitoa  na kusema kuwa ujenzi huo ulitakiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 180 na baada ya wao kupiga mahesabu wameona  gharama hiyo imepungua na kufikia kiasi cha shilingi milioni 140 kutokana na kupungua kwa gharama mbalimbali za ujenzi ikiwemo matofari kupatikana kiurahisi.
Wananchi wakiwa wanapewa maelekezo na viongozi wao kuhusu ujenzi wa maabara unavyoendelea katika shule ya sekondari Ukwiva.

Naye katibu Tarafa wa Tarafa hiyo ya Ulaya Raphael Mvurungu amesema kuwa jambo la ujenzi wa maabara ni la kila mwananchi na ni manufaa ya kila mwananchi kwani kwa kufanya hivyo hadi kufikia miaka ya mbele kutakuwa na wataalamu wa sayansi wa kutosha na amechukua hatua hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungabo wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuamua kujenga maabara kwa shule za sekondari.
                               wananchi wa kata ya ulaya wakiwa wanaangalia msingi wa maabara

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliokusanyika katika kikao hicho cha kusomewa mapato na matumizi Augustino Kikoti,Elia Dunia ,Asha Salehe na Abdallah Nassoro wameipongeza kamati ya ujenzi  kwa juhudi walizozifanya  hadi sasa na kutiwa moyo kwa kusomewa mapato na matumizi ambayo inaonyesha hali halisi ya fedha zao zilivyotumika na wameahidi kuendelea kuchangia ujenzi huo wa maabara hadi pale utakapokamilika
                                   kokoto ikiwa imekusanywa kwa ajili ya ujewnzi wa maabara

No comments:

Post a Comment