Diwani wa kata ya Ulaya Wilayani kilosa mkoani Morogoro
Raimond Chengula amewataka wananchi kuendelea kuchangia ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Ukwiva.
Wakwanza kushoto ni Diwani wa kata ya Ulaya Raimond Chengula wakatikati ni Afisa mifugo kijiji cha Mhenda piua ni mhasibu wa ujenzi wa maabara na wa mwisho ni Katibu Tarafa wa Tarafa ya Ulaya Raphael Mvurungu.
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wananchi
walipokuwa wanasomewa mapato na matumizi kuhusu ujenzi wa maabara ambao kwa
sasa umefikia hatua ya msingi ambapo Mhasibu wa kamati ya ujenzi Juma Khassim
amewasomea mapato na matumizi ya michango waliyoitoa na kusema kuwa ujenzi huo ulitakiwa kugharimu
kiasi cha shilingi milioni 180 na baada ya wao kupiga mahesabu wameona gharama hiyo imepungua na kufikia kiasi cha
shilingi milioni 140 kutokana na kupungua kwa gharama mbalimbali za ujenzi ikiwemo
matofari kupatikana kiurahisi.
Wananchi wakiwa wanapewa maelekezo na viongozi wao kuhusu ujenzi wa maabara unavyoendelea katika shule ya sekondari Ukwiva.
Naye katibu Tarafa wa Tarafa hiyo ya Ulaya Raphael Mvurungu
amesema kuwa jambo la ujenzi wa maabara ni la kila mwananchi na ni manufaa ya
kila mwananchi kwani kwa kufanya hivyo hadi kufikia miaka ya mbele kutakuwa na
wataalamu wa sayansi wa kutosha na amechukua hatua hiyo kumpongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungabo wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuamua kujenga maabara kwa
shule za sekondari.
wananchi wa kata ya ulaya wakiwa wanaangalia msingi wa maabara
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliokusanyika katika
kikao hicho cha kusomewa mapato na matumizi Augustino Kikoti,Elia Dunia ,Asha
Salehe na Abdallah Nassoro wameipongeza kamati ya ujenzi kwa juhudi walizozifanya hadi sasa na kutiwa moyo kwa kusomewa mapato
na matumizi ambayo inaonyesha hali halisi ya fedha zao zilivyotumika na
wameahidi kuendelea kuchangia ujenzi huo wa maabara hadi pale utakapokamilika
kokoto ikiwa imekusanywa kwa ajili ya ujewnzi wa maabara