Wakulima wilayani kilosa mkoani morogoro wametakiwa kuvitumia vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na mazazo yao pale wanapohitaji kuyauza.
Hayo yamesema katika mkutano mkuu wa kumi wa chama cha ushirika wilayani kilosa [kilosa co-operative union]KICU na muwakilishi wa mkuu wa wilaya Afisa utumishi mkuu wa wilaya ya kilosa Bw,Emmanuel .T. Nzunda akisoma hotuma iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya hiyo ya kilosa Adam Mgoyi na ameviomba vyama vya ushirika kuwapatia wakulima pembejeo za kilimo na madawa ya mazao yauhakika na ametoa onyo kwa wakulima kuacha kuchanganya mazao yao na mchanga hasa zao la ufuta kwani kwa kufanya hivyo kunashusha soko la biashara ya mazao na kushusha kipato katika wilaya pia amewahamasisha akina mama kujiunga na vyama vya ushirika ili kuleta chachu ya maendeleo katika sekta ya nzima ya ushirika.
Naye mwenyekiti wa mkutano huo Bw,Thadei Mnhangwi amewahamasisha wanawake,vijana na makundi yote kujiunga na chama cha ushirika ili kujipatia maendeleo kwa njia ya kushirikiana kwa sababu chama hicho kitawasaidia wakulima, kuuza mazao yao kwa bei nzuri na kuwahamasisha wakulima kujiunga na chama hicho, kwani wataweza kulima kilimo cha mkataba kilimo ambacho kitawasaidia wakulima kumudu gharama za kilimo na kuyauza mazao yao kiurahisi. Ameongeza kwa kusema kuwa kwa miaka hii, vyama vya ushirika vinaonekana kufifia na vingine kufa kwa sababu ya vyama hivyo kuingiliwa na siasa na kuwepo kwa soko hulia pia amewataka wakulima kuyatunza mazao yao vizuri mara baada ya kuyavuna ili kukuza soko la biashara ya mazao na kuyauza kupitia vyama vya ushirika ili kuwa na Takwimu kamili ya mazao yaliyouzwa.
Kwa upande wake meneja wa viwanda vya pamba vya ushirika wilayani kilosa Bw,Mohamedi Kindwiku amewaomba wakulima kujihusisha na kilimo cha pamba kwa kuwatia moyo kuwa kiwanda hicho kipo wilayani kilosa na mashine zipo.
Aidha Afisa kilimo Abel A.mchome aliyemwakilisha Afisa ushirika wilaya amewataka wanachama hao wao kuwa mstari wa mbele katika kilimo ili wawe mfano mzuri kwa wanachama wanaotakiwa kujiunga na ameahidi kutoa ushirikiano katika kuliendeleza shirika hilo.
Naye afisa ushirika mkoa wa morogoro Bi,Esther Kisiga amewaomba wajumbe kuyatekeleza yale yaliyoadhimiwa kwenye kikao na kuwaomba vijana kuwa mstari wa mbele kujiunga katika vyama vya ushirika ili kujipatia maendeleo na amewatoa wasiwasi wakulima kuwa masoko yapo hivyo amewahimiza kujitahidi katika kilimo.
Kwa upande wake mjumbe wa chama cha wakulima wa pamba Tanzania[TACOGA] Bi,Zena Kabonga amewaomba wanakilosa kulima zao la pamba na kuiomba serikali kuhusu pembejeo za kilimo hasa madawa kwani kuna baadhi ya dawa si nzuri haziui wadudu hivyo kusababisha kuendelea kuharibu mazao yao.
HII NI BLOG ITAKAYOKUKUTANISHA NA WANAHABARI MBALI MBALI WAKIKUHABALISHA NA KUKUJUZA YALE YANAYOTOKEA SEHEMU MBALI MBALI ZA DUNIA HII..KARIBU KWA KUFAHAMU MENGI ZAIDI KUPITIA HABARI.....
Friday, June 30, 2017
WAKULIMA WILAYANI KILOSA WATAKIWA KUJIUNGA NA VYAMA VYA USHIRIKA ILI KUJIPATIA MAENDELEO KWA NJIA YAKUSHILIKIANA
Friday, June 23, 2017
WAKAZI WA WILAYANI KILOSA KATA YAMAGUBIKE WAKABIDHIWA HATI MILIKI ZA KIMILA ZA KUMILIKI ARDHI KISHERIA
Wananchi wa kijiji cha magubike kilichopo wilayani kilosa mkoani morogoro wamekabidhiwa hati milki za ardhi kutoka Bodi ya Taifa ya mpango yakuasinisha rasilimali za biashara za wanyonge nchini MKURABITA.
Akikabidhi hati hizo kwa wananchi Mkuu wa wilaya ya kilosa Adamu Mgoli katika kijiji cha magubike kilichopo kata ya magubike baada ya bodi ya Taifa ya mpango wa kuasinisha Rasilimali za biashara za watu wanyonge nchini MKURABITA kuwaendea wakulima kisha kupima mashamba yao chini ya usimamizi wa uongozi wa serikali ya vijiji kwa lengo la kuepusha migogoro baina yao sanjali na kutumia hati hizo kujinufaisha kiuchumi.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kilosa Juma kesi Mkambala amewapongeza wananchi wamagubike kwa kupata hati miliki hizo kwani zitawasaidia kutatua migogoro ya ardhi kwani hati hizo zinaonesha mwanzo na ukomo wa eneo unalolimiliki.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya MKURABITA Kepteni mstaafu John Chiligati amesema bodi hiyo imeamua kuanzisha mchakato huo kwa sababu hati miliki za kimila kusudio ni kuhakikisha wananchi wananufaika kiuchumi na kuondokana na migogoro baina yao.