Friday, June 23, 2017

WAKAZI WA WILAYANI KILOSA KATA YAMAGUBIKE WAKABIDHIWA HATI MILIKI ZA KIMILA ZA KUMILIKI ARDHI KISHERIA

Wananchi wa kijiji cha magubike kilichopo wilayani kilosa mkoani morogoro wamekabidhiwa hati milki za ardhi kutoka Bodi ya Taifa ya mpango yakuasinisha rasilimali za biashara za wanyonge nchini MKURABITA.

Akikabidhi hati hizo kwa wananchi Mkuu wa wilaya ya kilosa Adamu Mgoli katika kijiji cha magubike kilichopo kata ya magubike baada ya bodi ya Taifa ya mpango wa kuasinisha Rasilimali za biashara za watu wanyonge nchini MKURABITA kuwaendea wakulima kisha kupima mashamba yao chini ya usimamizi wa uongozi wa serikali ya vijiji kwa lengo la kuepusha migogoro baina yao sanjali na kutumia hati hizo kujinufaisha kiuchumi.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kilosa Juma kesi Mkambala amewapongeza wananchi wamagubike kwa kupata hati miliki hizo kwani zitawasaidia kutatua migogoro ya ardhi kwani hati hizo zinaonesha mwanzo na ukomo wa eneo unalolimiliki. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya MKURABITA Kepteni mstaafu John Chiligati amesema bodi hiyo imeamua kuanzisha mchakato huo kwa sababu hati miliki za kimila kusudio ni kuhakikisha wananchi wananufaika kiuchumi na kuondokana na migogoro baina yao.

No comments:

Post a Comment