Monday, April 15, 2013

KINANA KUONGEA NA WAKAZI WA IFAKARA KESHO

Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi Taifa Bwana
Abdurahaman Kinana kesho
anataji kufanya ziara ya siku moja
Wilayani Kilombero na kuzungumza
na
Wananchi katika eneo la stendi ya
Kwa Makali.

Katibu wa siasa na uenezi CCM
Wilaya ya Kilombero Bwana
Pellegrine Kifyoga
ameiambia Habarikwanza kuwa
lengo la ziara hiyo ni
kuhamasisha ,kuangalia
utekelezaji wa ilani ya chama hicho
na kukagua uhai wa chama na
jumuiya
zake.

Bwana Kifyoga amesema kuwa
Bwana Kinana atafungua mashina ya
wakereketwa
na miradi ya kijamii na baada ya
hapo atazungumza na wananchi
pamoja na
wanachama wa CCM katika mkutano
wa hadhara utakaofanyika saa tisa
alasiri
katika Eneo la Stendi ya Kwa makali
Ifakara Mjini.

Katika Ziara ya Katibu huyo wa CCM
atambatana na Viongozi wa CCM
TAIFA, Katibu
wa NEC Itikadi na uenezi Bwana
Nape Nnauye na Katibu wa Nec
Oganaizesheni
Taifa Bwana Mohamed Seif  Khatib.

Amewataka wanachama na wananchi
kwa ujumla kujitokeza kwa wingi
kuwasikiliza
viongozi hao na kupokea maelekezo
yatakayotolewa na viongozi hao
katika
mkutano huo ili waweze kuyafanyia
kazi zaidi

No comments:

Post a Comment