SHILINGI BILIONI 3.3 KUTUMIKA KATIKA MLADI WA UMWAGILIAJI KILOMBERO .
JUMLA ya
Fedha shilingi Bilioni 3 Milioni 396 na Laki 9 na Elfu 9 Mia 2 na Tano zitatumika
kama Gharama ya Ujenzi wa Skimu ya
Umwagiliaji katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa Wilayani Kilombero.
Kwa muujibu
wa Taarifa ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero juu ya
Mradi wa Ujenzi wa Banio na Mfereji wa
Umwagiliaji imeeleza kuwa fedha
zilizopatikana mpaka sasa ni Milioni 510 Laki 2 na Elfu 61 Mia 3 na Sabini na
Tano Huku fedha zinazohitajika kukamilisha Ujenzi wa Skimu zikiwa ni Bilioni 2
milioni mia 916 Laki 6 na Elfu Arobaini na Saba Mia 8 na Thelathini na Tatu.
Taarifa
imefafanua kuwa kati ya fedha hizo shilingi Milioni 416 na Laki 4 Elfu Sitini
na Saba na Mia 3 Sabini na moja zimetumika katika Ujenzi wa Miundombinu Mfereji
Mkuu Mita 900, Mifereji ya Kati 3 Mita 925 na Maumbo mbalimbali 12.
Sehemu ya ujenzi wa mladi wa umwagiliaji wilayani kilombero
(picha na Henry Bernard Mwakifuna.)
Mradi huo
utakaosaidia upatikanaji wa uhakika wa Chakula na ongezeko la Kipato kuondokana
na Kilimo cha kutegemea Mvua utasaidia Kaya 1204.
Mradi huo
wenye eneo la Ukubwa wa Hekta 675 umepitia hatua mbalimbali tangu Mwaka 1975 ukiwa chini ya Wachina
walioanzisha Kituo cha Mafunzo ya kilimo ukipitia hatua mbalimbali unataraji
kukabidhiwa Mwishoni mwa Mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment