CHUO CHA
MTAKATIFU JOSEPH MOROGORO CHAFANYA TAMASHA LA MICHEZO ILI KUBORESHA MICHEZO NA
AFYA ZA WANACHUO.
Chuo cha
mtakatifu Joseph kilichopo mkoani Morogoro leo kimefanya tamasha la michezo katika viwanja
vya michezo vya chuo cha kilimo (Sua) kwa lengo la kuboresha michezo na afya za
wananchuo kupitia michezo .
Michezo hiyo
iliyoanza nyakati za asubuhi na kuhitimishwa saa kumi jioni ilihusisha pia
wanachuo kutoka katika chuo cha Morogoro
school of journalism (MSJ) ambapo michezo ya mpira wa miguu,mpira wa
pete,kuvuta kamba ,kukimbiza kuku,na mbio za mita mia nne kwa upande wa
wanafunzi na wakufunzi wao kutoa katika vyuo vyote viwili.
Mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya St Joseph Morogoro na Chuo cha habari morogoro(MSJ) Iliyoisha kwa ushindi wa goli 3(MSJ) kwa 1 St Josep (Picha na Beatrice Majaliwa)
Tamasha hilo
lilokuwa na lengo la kuwaweka wanafunzi katika hali nzuri kiafya ,kufahamiana
na kuweka mahusiano na ushirikiano baina ya vyuo shiriki.
Akisoma
hutuba kwa mgeni rasmi Rais wa wanachuo
kutoka katika chuo cha Mtakatifu Joseph bwana Emanuel Kabakeza amesema miongoni mwa chanagamoto
wanazokutana nazo katika michezo ni pamoja na upungufu wa vifaa vya michezo
ambavyo huwafanya kushindwa kufanya michezo yao kikamilifu.
Akijibu
risala hiyo wakati wa kufunga bonanza hilo mwakilishi wa mbunge wa Morogoro mjini ,katibu
wa mbunge huyo bwana Mourice Masala amesema kwa upande wake amefurahishwa na tamasha
hilo lilioandaliwa na chuo hicho na kusema kwa sasa chuo kimekuwa na umuhimu
mkubwa katika manispaa ya morogoro.
Masala amesema kuwa kwa sasa chuo cha mtakatifu
Joseph kimekuwa mkombozi kwa vijana wengi katika mkoa wa morogoro na mikoa mingine kwa
ujumla ikiwa ni sehemu mojawapo ya kupata taaluma katika fani mbalimbali.
Katika
kupunguza adha ya ukosefu wa vifaa vya michezo ofisi ya mbunge imetoa seti moja
ya jezi ya mchezo wa mpira wa miguu na mpira mmoja wa mchezp wa pete kwa
wasichana ili kuongeza ari ya michezo kwa wanachuo hao.