MBUNGE WA
MOROGORO MJINI MHESHIMIWA ABDUL AZIZ ABOUD AWATAKA WANAVYUO KUSHIRIKI MICHEZO
MBALIMBALI NA KUEPUKANA NA TABIA HATARISHI
Mbunge wa
morogoro mjini mheshimiwa Abdul Aziz Aboud amewataka vijana na wanavyuo waliopo
vyuoni kujishughulisha katika michezo ikiwa ni sehemu mojawapo katika afya ya mwanadamu.
Akizungumza
kwa niaba ya mbunge huyo katibu wake Bwana Mourice Masala amesema kuwa michezo ni muhimu kwa vijana na
hasa kwa wale waliopo vyuoni kwani huwafanya kuchangamsha miili yao na
kuepukana na kujiingiza katika vitendo viovu mara baada ya masomo yao.
Masala
ameyasema hayo wakati akifunga bonanza la michezo lililovishirikisha vyuo vya
Mtakatifu Joseph na Chuo cha uandishi wa habari MSJ vyote vya mkoani Morogoro.
Pia
amewahasa vijana wanachuo hao waliopo mafunzoni kuzingatia kwa makini mafunzo
yao ili waweze kuyahitimu kwa ufanisi na kuachana na tabia mbaya ambazo
zimekuwa zikifanywa na baadhi ya vijana ikiwemo kujjiingiza katika kutumia
madawa ya kulevya.
Nao wanachuo
hao walionesha ushiriki wao kikamilifu katika kushiriki kwao katika kufanya
michezo mbali mbali ambayo baadhi yake ilishirikisha wakufunzi kutoka katika
vyuo hivyo.
Na Beatrice Majaliwa
Morogoro
Na Beatrice Majaliwa
Morogoro
No comments:
Post a Comment