Wanakijiji wa ulaya mbuyuni
kata ya ulaya wilayani kilosa mkoani morogoro wameilalamikia serikali ya
kijiji na Tarafa kwa kutowatatulia mgogoro wao uliopo unaowahusu wafugaji
kuwavamia katika maeneo yao ya kilimo.
Mifugo ikiwa inashambulia zao la mbaazi
Wakitoa malalamiko yao kwa Jazba September 2 mwaka huu
kwenye mkutano wa kijiji ulioitishwa na Afisa Tarafa Baadhi ya wakulima katika
kijiji hicho cha ulaya mbuyuni Twist Twaha Kilabeba,Steven Mzuma na Omary
Mbwana alimaarufu kwa jina la [Gulamali] wamesema kuwa wamechoshwa na uongozi
uliopo madarakani hasa uongozi wa kijiji kwani umeonyesha dalili za kushindwa
kutatua mgogoro wao kwa muda mrefu hali ambayo inawafanya kukosa amani katika
mashamba yao na uhai wao kiujumla kwani wafugaji hao wa jamii ya kimasai
huwatishia wakulima hao.
Baadhi ya mazao aina ya mbaazi ikiwa imeharibiwa na mifugo aina ya ng'ombe
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo
amesema kuwa wafugaji waliokuwa maeneo ya wafugaji wanapaswa kuondoka haraka
sana kwani kisheria watakamatwa na kufunguliwa mashtaka na kuongeza kuwa
amewaagiza maafisa tarafa kwa ajili ya utekelezaji wa kuwaondoa wafigaji hao na
ameongeza kuwa wananchi hawapaswi kutoa maeneo yao kwa ajili ya kulisha mifugo
na badala yake wakibainika watakamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani na
kwa upande wa viongozi kama wakibainika kuwapokea wafugaji kinyemela
watawajibishwa kinidhamu kufunguliwa mashtaka mahakamani pamoja na kuwaondoa
madarakani.
Aidha Afisa tarafa wa Tarafa ya Ulaya Raphael Mvulungu
amewaomba wananchi kutuliza jazba zao na kuwaomba kutoa ushilikiano wao kwa
ajili ya kuwaondoa wafugaji hao wa jamii ya kimasai na kusema kuwa wafugaji hao
hawawezi kuleta ubishi wa kuondoka ila kutakuwa na watu watakao kuwa
wanawakingia kifua na kusema kuwa kuna baadhi ya wananchi wananufaika na
wafugaji hao na baadhi yao walimwambia wafugaji hao wasiondoke walipoambiwa
kuna mchakato wa kuwaondoa.
Aidha Mvulungu ameongeza kuwa katika zoezi la kuwaondoa
wafugaji hao ataanza na wale ambao wametoa maeneo yao kwa ajili ya kuwapa
wafugaji hao kwa ajili ya kujenga mazizi na wale wakulima ambao wanatoa maeneo
yao kwa ajili ya kulishia mifugo na kuongeza msisitizo kuwa atahakikisha
wafugaji hao wanaondoka katika kijiji hicho kikubwa amewaomba ushilikiano
wananchi kwa ajili ya kuwaondoa wafugaji hao.
No comments:
Post a Comment