Viongozi
wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa maslahi yao binafsi badala yake
wametakiwa kuwajibika kwa ajili ya maslahi ya wananchi na Taifa kwa
ujumla.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ukwiva
Hayo yamesemwa na Afisa tarafa wa tarafa ya ulaya
Raphael Mvurungu august 26 mwaka huu na amewataka viongozi kusimamia
miradi ya maendeleo katika maeneo yao ambapo amewataka viongozi wa Kata
ulaya kusimamia miradi hiyo ya maedeleo iliyokuwa viporo vya muda mrefu
katika maeneo yao hasa ujenzi wa nyumba za walimu ambao ni mradi wa muda
mrefu lakini bado hauja kamilika.
Baadhi ya majengo ya nyumba za walimu ambayo bado hayajamaliziwa katika ujezi wake
Aidha mkuu wa shule ya ukwiva Liberath Ngure ambapo ndipo
kwenye ujenzi wa nyumba za walimu ambazo hazimaliziki kwa ujenzi wake
amesema kuwa shule hiyo ya ukwiva inakabiliwa na changamoto nyingi
lakini lakini changamoto hizo hazifanyiwi kazi na viongozi na kusema
kuwa Mtendaji wa kata alishaahidi ahadi nyingi na hakutekeleza ahadi
hizo na kusema kuwa alishamuandikia barua tar 28/05/2014 kutoka katika
kamati ya ujenzi inayohusiana na ujenzi wa nyumba tatu [3] za walimu
ambapo ambayo barua hiyo ilikuwa ikimkumbusha kuhusu ujenzi wa nyumba
hizo lakini kukawa hakuna taarifa yoyote ya utekelezaji.
Mkuu wa shule ya ukwiva Liberath Ngure
Naye mwenyekiti wa kamati ya ujenzi shuleni hapo Timotheo
Mahembula amesema kuwa Halmashauri ilishatoa fedha kwa ajili ya
umaliziaji wa nyumba hizo lakini fedha hizo zilitumika kwa shughuli
nyingine jambo ambalo linaleta sitofahamu katika urudishaji wa fedha
hizo za umaliziaji wa majengo hayo na kuongeza kuwa Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya kilosa Amer Mubarack na alimwagiza mtendaji
kutafuta njia ya upatikanaji wa fedha ya umaliziaji wa nyumba hizo
lakini halmashauri ilishamaliza swala hilo la ujenzi wa
nyumba.
No comments:
Post a Comment