Jeshi la Polisi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro , Iimepiga marufuku Wananchi Jamii ya Kifugaji kuwatuma Watoto kuchunga Mifugo badala ya Kuwapeleka Shule kusoma.
Agizo hilo limetolewa Julai 24 Mwaka huu na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Wilaya ya Kilosa Afande Mayenga Thobiasi Mapalala Wakati akizungumza na HABARIKWANZA Ofisini Kwake kuhusiana na Swala hilo.
Afande Mapalala amesema kuwa kumekuwepo na Tabia kwa Baadhi ya Wafugaji kuwatumikisha watoto katika Kuchunga Mifugo badala ya kuwapeleka shule jambo linalowakosesha watoto hao haki yao ya msingi ya kupata Elimu ili waweze kuelimika na kuendeleza maisha yao.
Afande Mapalala amemuomba Afisa Elimu Msingi Wilayani Kilosa kufatilia suala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, ili kuwabaini Wazazi na Walezi ambao wanaacha kuwasomesha Watoto , na badala yake wanawatumikisha katika kuchunga Mifugo ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Aidha ametoa wito kwa jamii kutoa Taarifa kwa Afisa Elimu Msingi ama Jeshi la Polisi iwapo kuna Mzazi ama Mlezi anayeacha kumpelekeka Mtoto wake Shule na kumtumikisha katika kazi nyingine .
No comments:
Post a Comment