Saturday, April 22, 2017

WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA MBWADE WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO WAILALAMIKIA SERIKALI KWA KUTOKUWA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA KIJIJI

Wakazi wa kijiji cha mbwade wilayani kilosa mkoani morogoro wailalamikia serikali kwa kutokuwa na wenyeviti wa vitongoji na kusababisha kushuka kwa maendeleo katika kijiji Chao kwa kukosa wawakilishi katika vikao vya halmashauri ya kijiji.
Mmoja kati ya wakazi hao aliyeomba jina lake Lihifadhiwe amesema kuwa chanzo cha kijiji hicho kutokuwa na wenyeviti wa vitongoji nikutokana uchaguzi wa mwaka 2014 wa ngazi ya serikali ya mitaa kudai kuwa kuvamiwa nawatu ambao si wakazi wa kijiji hicho ambao walipiga kura jambo ambalo liliwafanya wakazi wa eneo hilo kugomea uchaguzi kutokana na watu hao kuonekana kupiga kura kuchagua mgombea kwa maslahi yao binafsi.

Kwa upande wake kaimu mtendaji wa kijiji hicho Huruma Kandili amesema kijiji hicho kina jumla ya vitongoji vitano ambavyo ni madoto lunch, mkwajuni, kichangani, usagarani, na mtapenda kati ya vitongoji vyote vitano kimoja kina mwenyekiti wa kitongoji ambacho ni kitongoji cha madoto lunch kwa upande wake amesema kuwa kijiji chake hakina wenyeviti wa vitongoji nikutokana na wanakijiji kuvunja masanduku yakupigia kura wakidai kuwa Kuna watu waliovamia uchaguzi ambao si wakazi wa kijiji hicho jambo ambalo amelikanusha na ameeleza kuwa watu hao ni wakazi wa kijiji hicho ila kijiji hicho kina jamii mbili ya wakulima na wafugaji hivyo jamii ya wafugaji watu wakuhama hama wakitafuta malisho yamifugo yao hivyo Muda wa uchaguzi walirudi kwa ajili yakufanya uchaguzi katika kijiji Chao.

Alipotafutwa mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya kilosa Kesi Juma Mkambala kuelezea ukweli wa taarifa hii amesema kuwa yeye hana taarifa kuhusiana na tatizo hilo na ameahidi kulifuatilia.

Thursday, April 20, 2017

KAYA 151 ZIMEATHILIWA NA MAFURIKO KATIKA KATA YA MVUMI WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO

Kaya takribani 151 zimeathilika na mafuriko katika kata mvumi wilayani kilosa mkoani morogoro mafuriko yaliyotokea alfajili ya april 20 mwaka huu na kuathili vitongoji viwili bomba kumi na mvumi A katika kata hiyo.
Akizungumzia hali halisi ya mafuriko hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilosa Kesi Juma Mkambala amesema mafuriko hayo yameathili kaya 151 na kati ya kaya hizo kaya 15 zimebomoka kabisa na wakazi kukosa mahali pa kuishi pamoja na taasisi mbili za serikali ikiwemo shule ya msingi mvumi A pamoja na ofisi ya kijiji kuvamiwa na mafuriko hayo.Ameongeza kwa kusema kuwa tayari serikali imetenga eneo kwa waathilika wa mafuriko hayo kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwapatia chakula huku kamati ya maafa ya wilaya ikiendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Akielezea chanzo cha mafuriko hayo mtendaji kata wa kata ya mvumi Aloyce izdoli amesema kuwa chanzo cha mafuriko hayo ni mto kisangata kujaa maji na kupasua na kuingia katika makazi ya watu na maji kukosa mahali pakutokea kutokana na eneo hilo kutokuwa na kalavati la kupitisha maji kwa kuwa eneo hilo kuna barabara ya lami itokayo dumila kuelekea kilosa hivyo maji kushindwa kupita kwenda upande wa pili wa barabara.

Baadhi ya wahanga wa mafuriko hayo Betha Magesa na Mashaka Rock wamesema kuwa athali walizozipata ni kubwa kutokana na mafuriko hayo kuingia ghafla na wao hawakuweza kuokoa vitu vyovyote katika makazi yao na baadhi yao kukosa mahali pakuishi kutokana na nyumba kubomoka na mazao kuingia maji.

Wednesday, April 19, 2017

BREAKING NEWS MAFURIKO YAWAVAMIA WAKAZI WA MVUMI WILAYANI KILOSA

Wakazi wa mvumi wilayani kilosa mkoani Morogoro waathirika na mafuriko yaliyotokea leo asubuhi na shughuli za uokoaji zinaendelea

Thursday, April 13, 2017

SIMBA YAIBUKA KIDEDEA KATIKA RUFAA YAO DHIDI YA KAGERA SUGAR

Simba wameshinda rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar na wamepewa point tatu baada ya kuibainika mchezaji wa kagera Sugar Mohammed Fakhi alicheza mechi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano katika michezo dhidi ya Mbeya City, Majimaji, African Lyon hizo ndio mechi ambazo amepata kadi za njano
Hivyo simba inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa na point 61 ikifuatiwa na waasimu wao yanga wakiwa na point 56

RUFAA YA SIMBA KUJULIKANA LEO

HATIMA ya rufaa iliyokatwa na Klabu ya Simba dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilimchezesha beki wake Mohammed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, inatarajiwa kujulikana leo baada ya kikao cha Kamati ya Saa 72 ya Usimamizi wa Ligi Kuu itakapokutana. 

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara namba 194, iliyofanyika Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-1. 

Taarifa kutoka kwa kiongozi mmoja wa bodi ya ligi (jina tunalihifadhi) ilieleza jana kuwa, kikao hicho kitafanyika leo kama ilivyopangwa na uamuzi juu ya rufaa hiyo utatolewa baada ya kikao hicho kumalizika. 

'Kikao kipo kama ilivyoelezwa, tayari maandalizi na nyaraka muhimu ambazo zilihitajika zimeshawasili, wajumbe wote wanaohusika wameshataarifiwa juu ya kuhudhuria kikao hicho," alisema kiongozi huyo wa bodi ya ligi. 

Kiongozi huyo alisema kuwa mbali na rufaa hiyo ya Simba, pia kikao hicho kitajadili taarifa za mechi nyingine mbili za ligi hiyo zilizofanyika juzi kwenye viwanja viwili tofauti hapa nchini. 

"Kikao kitajadili pia taarifa za mechi za juzi (Jumatatu) kati ya Mbao FC dhidi ya Simba na mchezo wa Mtibwa Sugar dhidi ya Azam FC, si unajua lazima nazo zijadiliwe kabisa kwa sababu tayari taarifa zimeshatumwa," aliongeza kiongozi huyo. 

Mechi ambazo Fakhi anadaiwa alionyeshwa kadi za njano ni ile iliyofanyika Desemba 17, 2016 katika mchezo namba 122 kati ya Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na nyingine ilikuwa ni Januari 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba, walipokipiga dhidi ya African Lyon ya Dar es Salaam. 

Machi 4, mwaka huu Fakhi alionyeshwa kadi nyingine ya tatu katika mchezo namba 190 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Kagera ilipoikaribisha Majimaji ya Songea. 

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alikaririwa na vyombo vya habari kuwa mchezaji huyo alikuwa na kadi mbili za njano na si tatu kama Simba wanavyodai.

Saturday, September 12, 2015

Dr WILBROAD SLAA AWAPIGA JIWE LINGINE CHADEMA




ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbrod Slaa amejitokeza hadharani kwa mara nyingine na kujibu watu waliojitokeza kuponda hotuba yake, aliyoitoa hivi karibuni kuwa hawana hoja zaidi ya kumtukana.

Akizungumza kupitia kituo kimoja cha Televisheni jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema madai yote, yaliyotolewa juu yake na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa Chadema na vyama vinavyounda Ukawa, baada ya hotuba aliyoitoa, hayana msingi wowote na kwamba ni kuishiwa hoja, ndio maana walimtukana badala ya kujibu hoja.

“Nashukuru hoja zangu zote hawajazijibu, sasa wanapiga tu propaganda, hata Rostam Aziz alijaribu kujibu, lakini akatukana tu kama alivyonitukana mwaka 2007 badala ya kujibu hoja na mimi nasema ufisadi ni hoja,” alisema Slaa.

Aidha, Dk Slaa alisema hawezi kumpeleka mahakamani Rostam ambaye ni kada wa CCM, ambaye amemtaka Dk Slaa ampeleke mahakamani kama anao ushahidi kuwa anaunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Slaa amesema yuko tayari kutoa ushahidi wake pale Jamhuri itakapomfungulia mashitaka. “Wale ambao hawaelewi taratibu za kesi, kuna kesi za madai ambapo mtu binafsi anafungua kesi na kesi za jinai ambazo mtu binafsi hawezi kufungua ila Jamhuri, kesi za Jamhuri mtu huwezi kufungua, wewe ni shahidi… mimi nikiitwa nitakwenda kutoa ushahidi dhidi ya Rostam Aziz,” alisema Dk Slaa.

Aidha, alisema ni kweli vijana wanataka mabadiliko na ni hoja ya msingi na pia wakulima ambao hawafaidiki na kilimo chao, wanataka mabadiliko, vivyo hivyo kwa makundi mengine.
 
 “Nimesema mimi Lowassa hafai, leo, lini ameanza kuwa rafiki wa masikini?

"Lini ameanza kuwa safi?Watanzania waache ushabiki usiofaa wapime kwa vigezo, ushabiki usio na tija utatuangamiza,” alisema Dk Slaa, akijibu hoja mbalimbali ambazo zimejitokeza baada ya hotuba yake hiyo, aliyoitoa mwanzoni mwa wiki hii baada ya kutangaza kuachana na mambo ya siasa na kubaki mshauri wa wananchi.

Akijibu shutuma dhidi yake baada ya kutuhumiwa kutoa habari za upotoshaji juu ya maaskofu, Slaa alisema alichokieleza siku ile anatangaza kujiengua kwenye siasa ni alichoambiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwamba maaskofu 30 kati ya 34 walihongwa.

“Tatizo halikuwa fedha bali askofu anaona sifa mimi kumuunga mkono mtu ambaye alitumia fedha kununua maaskofu, na Watanzania nawaomba mtulie msikurupuke na maneno bila kuyachambua, taifa linaangamia kwa sababu ya ushabiki usio na tija, nimeshtushwa na kauli yake, kiongozi anayepaswa kukemea rushwa, maovu… baba askofu piga magoti Mungu wako atazame dhamira yako,” alisema.

Dk Slaa alisema yeye ana uwezo wa kupambanua siasa na mambo mengine na kwamba ni kweli alikutana na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe katika Hoteli ya Serena na hiyo ni katika kupata taarifa alizozihitaji kwa ajili ya kazi yake ya utafiti na kwamba Mwakyembe ni chanzo cha taarifa cha kwanza na kwamba hakufanya kwa siri.

Akizungumzia picha yake ambayo ilizunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha yeye akiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema picha hiyo ni wakati wa mkutano wa vyama vya siasa na Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck alipokuja kwenye ziara ya kikazi Februari mwaka huu.

“Kwenye picha hizo ambazo zinatuonesha mimi, Mwigulu na Profesa Lipumba tukimpokea Rais wa Ujerumani alipotembelea Tanzania, leo ndio zinaletwa kuonesha eti haya ndiyo mazungumzo ya kumng’oa Slaa, naomba niwaambie warudi nyuma waangalie hizo picha ni za lini hazina uhusiano na mimi kujiondoa,” alisema Dk Slaa.

Aidha, Dk Slaa alisema kuwa kuna propaganda nyingine ambayo imetumika ambapo watu wametuma pia picha ambazo zinamuonesha akiwa kwenye ndege, ikisemekana kwamba ametoroka nchini baada ya hotuba, sio kweli.

Alikiri kusafiri lakini sio kwa kutoroka, kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu na kwamba amekuwa akipiga picha na watu kwenye ndege na kwamba picha hiyo ni ya safari ambayo alishasafiri na kurudi.

“Magazeti na mitandao wanasema Dk Slaa hayuko nchini, lakini nadhani sasa Watanzania wanaona sasa niko hapa studio Dar es Salaam na siko Marekani,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa uongo huo unaonesha ni aina gani za siasa zilizopo hapa nchini.


Alisema hoja ya wapi amepata fedha kwenda Serengeti na kuishi hotelini ni hafifu. “Nilikwenda Marekani na kukaa kwa zaidi ya miezi 12 na kutembelea majimbo 13 na sikulipiwa na mtu yoyote zaidi ya chama changu kulipia shilingi 500,000 kwa mshauri aliyeandaa nyaraka ya kunisaidia katika ziara hiyo, mbona hawakuniuliza nimepata wapi fedha hizo?”

wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema na chama cha mapinduzi ccm wapigana na kusababisha mauaji




Wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), juzi walishambuliana kwa ngumi na silaha za jadi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine watano.

Tukio hilo limetokea saa 4.09 asubuhi katika Kijiji cha Mangucha, Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wanachama na wafuasi wa vyama hivyo wakiwa kwenye shughuli za kampeni za vyama vyao. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa, alisema chanzo cha vurugu hizo ni mapambano yaliyohusisha silaha za jadi baada ya wafuasi wa Chadema kufanya maandamano ya kwenda kuwapokea wagombea ubunge na udiwani waliokuwa wakitokea Kijiji cha Mwambara kwenda Kijiji cha Kegonga ambako pia kulikuwa na mkutano wa kampeni za CCM.

Kamanda Mambosasa alisema wafuasi wa Chadema walipofika eneo ambalo wana CCM walikuwa wakifanya mkutano wao walinyoosha mikono juu huku wakionyesha alama ya vidole viwili ambayo huitumia kwa salamu kitendo ambacho kiliamsha hasira za wafuasi wa CCM na ndipo mapambano hayo yalipotokea.

Alimtaja aliyeuawa katika mapambano hayo kuwa ni Mwita Bhoke Waite (37) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyandage baada ya kushambuliwa na kitu chenye ncha kali kifuani na kwenye paja la mguu wa kushoto.

Kamanda Mambosasa aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Chacha Mwita Chacha (32) mkazi wa Kijiji cha Nyasage ambaye alijeruhiwa mgongoni, mguuni na mkononi, Kimunye Chacha Mgesi (54) mkazi wa Kegonga aliyejeruhiwa mikono yote miwili na kichwani pamoja na Elizabeth Wiliam Marwa (43) ambaye ni mtumishi wa CCM Wilaya ya Tarime alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa kupigwa na ubapa wa panga.

Majeruhi wengine aliowataja ni Oueen Ryoba (47) ambaye ni mfanyabiashara aliyejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa kupigwa na ubapa wa panga na Nyaitati Marianya (30), mkazi wa Kegonga aliyejeruhiwa mkononi.

Akizungumzia mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Kamanda Mambosasa alisema Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanne wanaotuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Kius Matiko (28) mkazi wa Kijiji cha Kegonga, Nyambari Nchagwa (43) mkazi wa Kijiji cha Nyandage, Marwa Samweli (25) na Magasi Samweli Ghati, wote wakazi wa Kijiji cha Kegonga Wilaya ya Tarime.

Naye Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Tarime, Rose Hosea, alipoulizwa kuhusu hali za majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo alisema wanne wanaendelea vizuri na matibabu isipokuwa mmoja aliyemtaja kwa jina la  Chacha Mwita Chacha ambaye  amehamishiwa Hospitali ya Musoma kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.

Wakati huo huo, taarifa zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni zimeeleza kuwa gari la mgombea ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko limeharibiwa vibaya katika mapambano hayo.


Alisema gari hilo lenye namba za usajili T 282 DEE lilishambuliwa kwa mawe wakati wa mapambano hayo yakiendelea na imekuwa vigumu kutambua mara moja waliohusika na uharibifu huo.

Monday, December 8, 2014

WANANCHI WA WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO WATAKIWA KUWA MAKINI KWA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA KIJIJI KWA KUCHAGUA KIONGOZI ATAKAYEJALI MASLAHI YA WANANCHI



Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo amewataka wananchi wa wilayani kilosa kuwa makini kwa kipindi hiki cha kampeni kwa kuwachagua viongozi watakaojali maslahi yao. 
                                   Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo akiwa ofisini kwake.

Ameyasema hayo December 8 mwaka huu wakati akizungumza na HABARIKWANZA  ofisini kwake kuhusiana na hali ya kampeni inavyoendelea wilayani kilosa na ameeleza kuwa hali ya kampeni inaendelea vizuri na kwa amani.
Mh:Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo akiwa anaongea na HABARIKWANZA ofisini kwake

Aidha amewataka viongozi wanaofanya kampeni kutumia lugha nzuri zisizo za matusi kwani siasi haiendeshwi kwa matusi na amesema kuwa mwanasiasa anayetumia lugha chafu za matusi huyo hajakomaa kisiasa na hana sera ya kuwaambia wananchi ili wamchague.

Pia Tarimo amewataka wananchi kusoma katiba mpya ambayo inatakiwa kupigiwa kura na amewataka wananchi kuwa makini pindi zitakaposambazwa kwa kuweza kuipigia kura pasipo kushawishiwa na mtu au kikundi cha watu kitu  ambacho kitamfanya mwananchi kuipigia kura pasipo ridhaa yake (kushawishiwa) na amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuipigia kura katiba hiyo pindi muda wake utakapofika.

Monday, October 27, 2014

UJENZI WA MAABARA WAPAMBA MOTO



Diwani wa kata ya Ulaya Wilayani kilosa mkoani Morogoro Raimond Chengula amewataka wananchi kuendelea kuchangia ujenzi  wa maabara katika shule ya sekondari Ukwiva.
Wakwanza kushoto ni Diwani wa kata ya Ulaya Raimond Chengula wakatikati ni Afisa mifugo kijiji cha Mhenda piua ni mhasibu wa ujenzi wa maabara na wa mwisho ni Katibu Tarafa wa Tarafa ya Ulaya Raphael Mvurungu.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wananchi walipokuwa wanasomewa mapato na matumizi kuhusu ujenzi wa maabara ambao kwa sasa umefikia hatua ya msingi ambapo Mhasibu wa kamati ya ujenzi Juma Khassim amewasomea mapato na matumizi ya michango waliyoitoa  na kusema kuwa ujenzi huo ulitakiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 180 na baada ya wao kupiga mahesabu wameona  gharama hiyo imepungua na kufikia kiasi cha shilingi milioni 140 kutokana na kupungua kwa gharama mbalimbali za ujenzi ikiwemo matofari kupatikana kiurahisi.
Wananchi wakiwa wanapewa maelekezo na viongozi wao kuhusu ujenzi wa maabara unavyoendelea katika shule ya sekondari Ukwiva.

Naye katibu Tarafa wa Tarafa hiyo ya Ulaya Raphael Mvurungu amesema kuwa jambo la ujenzi wa maabara ni la kila mwananchi na ni manufaa ya kila mwananchi kwani kwa kufanya hivyo hadi kufikia miaka ya mbele kutakuwa na wataalamu wa sayansi wa kutosha na amechukua hatua hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungabo wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuamua kujenga maabara kwa shule za sekondari.
                               wananchi wa kata ya ulaya wakiwa wanaangalia msingi wa maabara

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliokusanyika katika kikao hicho cha kusomewa mapato na matumizi Augustino Kikoti,Elia Dunia ,Asha Salehe na Abdallah Nassoro wameipongeza kamati ya ujenzi  kwa juhudi walizozifanya  hadi sasa na kutiwa moyo kwa kusomewa mapato na matumizi ambayo inaonyesha hali halisi ya fedha zao zilivyotumika na wameahidi kuendelea kuchangia ujenzi huo wa maabara hadi pale utakapokamilika
                                   kokoto ikiwa imekusanywa kwa ajili ya ujewnzi wa maabara

Wednesday, October 1, 2014

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHA SIMAMA IMARA KWA KUPATIKANA KWA HAKI KWA KILA MWANANCHI



Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC mwishoni mwa wiki iliyopita kimetimiza umri miaka 19 toka kuanzishwa kwake.
 Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliohudhulia katika sherehe za kutimiza miaka 19 ya kituuo cha kutetea haki za Binadamu LHRC Jijini Dar es salaam.
Katika sherehe hiyo ya kusheherehekea miaka 19 toka kuanzishwa kwake yaliyohudhuliwa na mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania Jaji Joseph Walioba pamoja na viongozi mbalimbali kwa ngazi za kisiasa na kiserikali.
Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko Jaji Joseph Warioba akiongea wakati wa maazimisho hayo ya 19 ya kituo cha wasaidizi wa kisheria.

Katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 19 toka lianzishwe shirika hilo la kutetea haki za binadamu Walioba ameliomba shirika hilo kusimama imara kwa kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki yake stahiki hasa

                 Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Bi,Helen Kijobi Simba
 kipindi hiki cha mchakato wa kupata katiba mpya amesema kuwa wananchi wanapaswa kutambua katiba ili inapofika wakati wa kuipigia kura wajue wanaipigia kura katiba ipi.
Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Waroba akifuatiwa na Mkurugenzi wa kituo cha usaidizi wa kisheria Bi,Helen Kijobi Simba akifuatiwa na Askofu

Aidha Warioba amewataka wasaidizi wa kisheria kuwapa elimu wananchi waliopo vijijini na mjini ili kuhakikisha wananchi walio wengi wanajitambuana kutambua umuhimu wao katika jamii na Taifa kiujumla.
 Baadhi ya wasaidizi wa kisheria kutoka wilayani Serengeti wakipokea zawadi baada ya utendaji mzuri wa kazi zao
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo la kutetea haki za binadamu nchini Tanzania LHRC Helen Kijobi Simba amesema kuwa katika utendaji wao wa kazi wakiwa wasaidizi wa kisheria wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo wanasiasa kuingilia katika utendaji wao wa kazi na kuonekana wasaidizi wa 

Mwenyekiti wa chama cha CUF Prof;Ibrahim Lipumba[kushoto] akiwa na mmoja na wajumbe katika Tamasha la miaka 19 ya kituo cha sheria na haki za binadamu.


kisheria kama wapinga maendeleo na kuwa kikwazo jambo ambalo Bi,Simba amesema ni kikwazo kikubwa kwao katika ufanyaji wa kazi.
Inayoonekana kwa mbele ni keki iliyoandaliwa katika tamasha la kituo cha sheria na haki za binadamu. 

Aidha Bi,Simba amewataka wasaidizi wa kisheria kutokata tamaa katika kutetea haki za wananchi ambao hawajui hata pakuanzia.