Wednesday, December 8, 2010

BEI KUBWA YA MBOLEA YAWA KIKWAZO KWA WAKULIMA WILAYA YA NJOMBE

MBOLEA ZAWA KIKWAZO KWA WAKULIMA ,NJOMBE.

Wananchi Wilayani Njombe Wameendelea kulalamikia Bei Kubwa ya Mbolea licha ya serikali kutangaza kuwa Zingeuzwa kwa punguzo kufuatia kuwepo kwa Utaratibu wa Malipo ya Ruzuku

Katika Vijiji vya Lupembe,Tarafa za Makamabako na Maeneo ya Ilembula Wananchi Wamelalamikia Kuuziwa Mbolea Hizo kwa bei ya juu Zaii Toafuti na Walivyoelekezwa hapo Awali

Wakiongea na mtandao huu baadhi ya wananchi wamesema mbolea aina ya DAP kwa madukani inauzwa 65 elfu kwa ruzuku wananunua kwa shilingi 39 elfu ambapo serikali inakua imelipia kiasi cha 26 elfu.Kwa upande wa mbegu,wamesema kwa kilo 10 ya luzuku inauzwa 20 elfu na madukani inauzwa 40 elfu.

Hali Hio Imewafanya Wananchi hao Wasione Umuhimu wa kuwepo kwa Ruzuku hio kwani Bei Inayouzwa Madukani Wamedai kutotofautiana na Bei inayouzwa na Mawakala wa Ruzuku

Licha ya Malalamiko hayo lakini Bado Wananchi hao Wameelezea jinsi Zoezi hilo linavyoendeshwa kwa madai ya kuendeshwa katika hali ya Taratibu hali ambayo inawachelewesha kuanza Msimu Mpya wa Kilimo Ambao Unakaribia kuanza

Mmoja wa Mawakala wa mbolea CLEA MGINA, amesema sababu za kuchelewa kumaliza zoezi hilo ni Kutokana na gharama kubwa za Ununuzi wa Mbolea Hizo hivyo wananchi wanashindwa kulipia kwa Wakati gharama hizo.

No comments:

Post a Comment