KANISA LAWAKUMBUKA WAUMINI WAKE NA KUAMUA KUTOA HUDUMA YA UMEME KWA WANANCHI NJOMBE.
Wakati Wananchi wakipata Hadha kubwa kutokana na Kukatizwa Katizwa kwa Huduma ya Umeme Mara kwa Mara Sasa Hali hio huenda Ikawa Historia Baada ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe Kuanza Kutoa Huduma ya Umeme kwa Bei Nafuu Tofauti na Ile inayotozwa na Shirika la Ugavi Tanzania TANESCO
Katika Kutatua Kero kwa Njia Iliosahihi Zaidi ya Wakazi 250 Wameripotiwa kuanza kunufaika na Huduma hiyo ambayo pia itawaunganisha Wakazi wa Ludewa.
Askofu wa jimbo hilo Mhashamu Alfred Maluma amesema lengo la mradi huo ni kuwapa nyenzo ya kuondokana na umasikini kutokana na maeneo ya vijiji ambavyo viko katika mazingira magumu ya kufikiwa na maendeleo yanayofanywa na Serikali.
Akizungumzia Mradi Huo wa umeme wa Mawengi wilayani Ludewa unaoendeshwa na kanisa Katoliki Jimbo la Njombe Askofu huyo Amesema Mradi huo pia umeanza kusambaza umeme kwa wananchi kwa bei nafuu kuliko inayotozwa na Shirika la Umeme (Tanesco).
Askofu Maluma alikuwa akizungumza na kundi la wanahabari waliotembelea mradi huo ambao umejengwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la ACRA chini ya ufadhili wa Serikali ya Italia.
Kwa mujibu wa Katibu wa Huduma za jamii na Maendeleo wa kanisa Katoliki jimbo la Njombe, Padri Evodius Msigwa wananchi ambao wameunganishiwa umeme hadi sasa wanafikia 250 na juhudi zinaendelea kuwaunganishia wengine.
Padri Msigwa ambaye ni Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Njombe alisema kutokana na wananchi wengi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za kuunganisha umeme, jumuiya ya Lumama inawatoza asilimia 20 ya maunganisho na asilimia 80 wanalipa kidogo kidogo ndani ya mwaka mmoja.
Umeme huo unaozalishwa kwa kutumia maporomoko ya maji kama ilivyo kwa vyanzo vingine vya Tanesco, unahudumia vijiji vitatu vya Mawengi, Lupande na Madunda na una uwezo wa kuzalisha kilowati 150 kwa siku.
Askofu huyo alisema ili umeme huo uweze kuwafikia watu wengi katika vijijini vingine, ni lazima Serikali ishirikiane kwa karibu na kanisa hilo, wahisani pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) ili kuusambaza kwa wananchi wengi zaidi kutokana na miundombinu yake kuwa aghali.
No comments:
Post a Comment