Halmashauri
ya kijiji cha chanzuru wilayani kilosa mkoani morogoro inatarajia kukusanya
kiasi cha shilingi milioni Thelathini na moja laki tatu na arobaini elfu kwa
ajili ya maendeleo ya kijiji.
Hayo
yamesemwa mapema mwanzoni mwa wiki hii na mtendaji wa kijiji hicho salumu
kibugula wakati akiongea kwenye mkutano wa wananchi na viongozi wa kijiji hicho
alipokuwa akisoma bajeti ya mapato na matumizi ya nusu ya mwaka wa fedha
2013/2014.
Kibagula
amesema kuwa katika bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2013/2014 kijiji kinatakiwa
kukusanya kiasi cha shilingi milioni ishirini na moja laki tatu na Arobaini
kupitia vyanzo vyake vya ndani na shilingi milioni kumi kutoka kwa wahisani na
ruzuku ya halmashauri ya wilaya kilosa.
Katika
mkutano huom pia kumejadiliwa mgogoro wa mashamba kati ya mwekezaji
aliyefahamika kwa jina la Bahamisi na wananchi wa kijiji hicho kuhusiana na
mipaka iliyowekwa na idara ya ardhi wilayani kilosa
No comments:
Post a Comment