Mbunge wa
jimbo la mikumi mkoani morogoro Abdulsalama Amer amewataka vijana waendesha
pikipiki za kubeba abiria maarufu kama bodaboda kuunda vikundi ili waweze
kupatiwa mkopo wa pikipiki zitakazowawezwsha kujikwamua kiuchumi.
Abdulsalama
maarufu kwa jina la sas gesametoa wito huo kwa vijana wa jimbo lake la mikumi
wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha kitete
msindazimapema wiki hii wakati wa ziara yake kwenye kijiji hicho kilichopo
kwenye kata ya Ruhembe wilayani kilosa.
Sas gas
amesema kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na kampuni husika itakayotoa mikopo
hiyo na sasa kinachosubiriwa ni vijana hao kuunda vikundi na kufuata taratibu
zinazotakiwa ili waweze kukopeshwa.
Mbunge huyo
amesema mikopo hiyo itawasaidia vijana hao kupata pikipiki na wataweza kuacha
kuendesha pikipiki za matajiri wao na kuendesha za kwao kitu ambacho
kitawasaidia kijikwamua kiuchumi.
Wakiongea
vijana hao wamesema kuwa wanampongeza mbunge wao kwa jitihada hizo kwani
watakapokopeshwa hizo pikipiki zitawasaidia kupata pesa na kuweza kutimiza
ndoto zao za maisha bora kwa upande wao.
No comments:
Post a Comment