Mbunge wa jimbo la kilosa Mustafa Haidi mkulo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezajiwa miradi ya maendeleo katika kata za Lumuma na kidete wilayani klilosa.
Akiwa katika ziara hiyo,Mkulo aliongozana na katibu wa wazazi wilaya Abdul Gombe na wataalamu mbalimbali kutoka wilaya ya kilosa.
Katika kata ya kidete Mbunge mkulo amekagua mradi wa ujenzi wa bwawa la kidete ambalo hadi sasa halijakamilika tangu mwaka 2010 ulipoanza,Sababu ikiwa ni kutowaingizia pesa inayosimamia mradi huo wa ujenzi wa bwawa.
Aidha amekagua mradi wa uchongaji wa barabara wa lumuma-kibasingwa yenye urefu wa kilometa nane ambayo imechongwa kilometa sita hadi sasa barabara hiyo imechongwa na mfuko wa jimbo wa mkulo,ambapo mbunge huyo ameahidi kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia kilometa mbili zilizobaki.
Mbunge mkulo amefanya ziara hiyo January 6 n January7 ambapo pia ameweza kutembelea mradi wa barabara ya lumuma Mnozi ambayo haijakamilika hadi sasa na mbunge huyo ameahidi kuwa barabara hiyi itaanza kuchongwa mapema hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment