Jumla ya vitabu arobaini na saba elfu na thelathini February
13 mwaka huu vimetolewa kwa shule za
sekondari wa kumi na tisa wilayani
kilosa na shule sita wilaya mpya ya Gairo.
Vitabu hivyo vimetolewa na shirika la camfed ambalo
linashughulikia kwa kuwasaidia watoto walio mashuleni wasio na uwezo licha ya
kutoa vitabu na vifaa vingine mashuleni ,pia shirika hilo hutoa karo za shule
na mavazi kwa wanafunzi hao.
Akikabidhi vitabu hivyo kwa mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya kilosa Amer Mbaraka Afisa
mradi wa kamfed ambaye pia ni mlezi wa kafed mkoani morogoro Deogratius john
amesema kuwa kamfed imedhamilia Nyanja
ya elimu ili kufanikisha mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa yaani [BRN].
Kati ya vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Dunia yangu bora,How
to read English,English study guide,mathematical study guide na biology
studyguide
Pia bwana Deogratius John amewataka walimu kupanga mkakati bora
kwa kila mwanafunzi apate vitabu hivyo na kuvitumia ipasavyo.