Friday, February 14, 2014

KIVUMBI CHA LIGI DARAJA LA KWANZA KUENDELEA KUTIMKA KESHO KATIKA VIWANJA TOFAUTI NCHINI


( PICHA BY PETER LAURENCE )
                                            
Timu ya polisi Morogoro imeondoka jana kuelekea Iringa ikiwa tayari kwa mchezo wa ligi daraja la kwanza  dhidi ya LIPULI ya mkoani humo,  mchezo utakaochezwa jumamosi ya Februari 15 katika uwanja wa Samora Iringa.


Meneja wa timu hiyo ya polisi  Fikiri Husein ameiambia HABARI KWANZA BLOG kuwa  timu yake imejiandaa vizuri na itaibuka na ushindi katika mchezo huo huku akiwatupia lawama waamuzi kuwa ndio chazo cha wao kutofanya vizuri katika michezo yao ugenini.

Timu ya polisi morogoro inaongoza kundi B ikiwa na jumla pointi 18 huku Lipuli ikiwa na pointi 9.
 mchezo huo mkali wa kukata na shoka utafanyika tarehe 15 kwenye uwanja wa Somara Iringa, Wakati huo huo Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri  Bukina Faso maarufu kwa jina timu ya wananchi watawakaribisha Mkamba Rangers kutoka Kilombero.

No comments:

Post a Comment