Friday, February 21, 2014

RT WAWASILISHA MAJINA 40 YA WANARIADHA KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE.

Shirikisho la Riadha Tanzania limewasilisha majina 40 ya wanariadha na sita ya walimu kwenye ofisi ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa tayari kwa ajili ya timu ya taifa ya riadha  kushiriki katika  mafunzo  nje ya nchi.

Rais wa shirikisho la riadha Tanzania Anthony Mtaka amesema wameamua kuwasilisha majina hayo mara baada ya wizara hiyo  kuchukua jukumu la kuwapeleka wanariadha hao nje ya nchi kwenda kujifunza ili baadaye waiwakilishe vema nchi katika mashindano ya Kimataifa.
Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa inachukua jukumu la kuwapeleka wachezaji 40 na walimu 6 katika nchi za China, Uturuki na Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya jumuiya ya madola.

Kwa upande wao wadau mbalimbali wa michezo wameipongeza serikali kwa  uamuzi huo wa kuwapeleka wanariadha hao nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kujifunza.

Safari hiyo kwa timu ya taifa ya riadha imekuja katika wakati muafaka kwani itaisadia timu hiyo kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya michuano ya kimataifa ya jumuiya ya madola inayotarajia kufanyika huko  Scotland Julai 23 mwaka huu.



No comments:

Post a Comment