Mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri ya wilaya ya kilosa masalu mayaya,ametakiwa kuwaita
walimu wote wa wilaya ya kilosa ili kuweza kuwaeleza matatizo yao na
kuyatafutia ufumbuzi.
Wito huo umetolewa Februari 13 mwaka huu na mwenyekiti wa
halmashauri wa wilaya kilosa mheshimiwa Amer Mubarak katika kikao cha kamfed
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo wakati kamfed
ilipokuwa ikikabidhi vitabu vya wanafunzi wa sekondari .
Mubarak emesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kujua
matatizoyanayowakabili na kuyatafutia ufumbuzi,lengo likiwa ni kuongeza ufaulu
mashuleni.
Pia amezitaka bodi za shule kuwa makini nakupa ulewa wa matatizo yashule zao na kujaribu kutatua
na ikishindikana wafike wilayanikuomba nsaada.
;
Aidha mwenyekiti wa halmashuri hiyo ametaka wananchi
wahamasishwe kujenga nyumba za walimu karibu na shule ili kuwapa wepesi katika
kufanya kazi yao ya kufundisha.
No comments:
Post a Comment