Watafiti kutoka chuo
kikuu cha Sokoine SUA wamefanya utafiti Wilayani Kilosa katika mpango wa
kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa inayetokana na ukataji miti ovyo na uhalibifu
wa misitu (MKUHUMI) katika vijiji vitano vinavyotekeleza mradi huo wilayani Kilosa.
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa misitu wilayani
Kilosa march 24 mwaka huu na wawakilishi wa vijiji hivyo mfadhili wa chuo kikuu
cha Sokoine SUA Santos Silayo amesema
kuwa wameanzisha mradi huo kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya
nchi na mradi huo umeanzisha katika
wilaya tatu ambazo ni Kilosa , Rungwe na Kondoa
lengo likiwa ni kuwaelimisha wananchi
juu ya matumizi bora ya ardhi
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo amewaomba
wahadhiri na wasimamizi wa mradi huo wa
MKUHUMI kuwaelimisha wananchi juu ya changamoto wa uharibifu wa misitu kwa
kusema kuwa imeshamili maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kilosa ambapo watu
wanaharibu misitu hiyo na kutochukuliwa hatua kupitia sheria za hifadhi ya
misitu katika vijiji hivyo na kuendelea na uharibifu wa misitu hiyo.
Aidha kwa upande wake Diwani kata ya Lumbiji Herman Msafiri ameupongeza mradi huo wa
MKUHUMI kwani wameweza kupata elimu kuhusu matumizi bora ya ardhi . Pia amesema
kuwa wanaushukuru mradi huo kwa kuwaelimisha juu ya shughuli za mashambani
kupewa elimu ya shamba darasa kwa kufundishwa mbinu za kilimo hifadhi na kilimo
rafiki.