Wednesday, March 26, 2014

WILAYA YA KILOSA YANUFAIKA NA MRADI WA MKUHUMI KUHUSU KUPAMBANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA



Watafiti  kutoka chuo kikuu cha Sokoine SUA wamefanya utafiti Wilayani Kilosa katika mpango wa kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa inayetokana na ukataji miti ovyo na uhalibifu wa misitu (MKUHUMI) katika vijiji vitano vinavyotekeleza  mradi huo wilayani Kilosa.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa misitu wilayani Kilosa march 24 mwaka huu na wawakilishi wa vijiji hivyo mfadhili wa chuo kikuu cha Sokoine SUA Santos  Silayo amesema kuwa wameanzisha mradi huo kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya nchi  na mradi huo umeanzisha katika wilaya tatu ambazo ni Kilosa , Rungwe na Kondoa  lengo likiwa ni kuwaelimisha wananchi  juu ya matumizi bora ya ardhi

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo amewaomba wahadhiri  na wasimamizi wa mradi huo wa MKUHUMI kuwaelimisha wananchi juu ya changamoto wa uharibifu wa misitu kwa kusema kuwa imeshamili maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kilosa ambapo watu wanaharibu misitu hiyo na kutochukuliwa hatua kupitia sheria za hifadhi ya misitu katika vijiji hivyo na kuendelea na uharibifu wa misitu hiyo.

Aidha kwa upande wake Diwani kata ya Lumbiji  Herman Msafiri ameupongeza mradi huo wa MKUHUMI kwani wameweza kupata elimu kuhusu matumizi bora ya ardhi . Pia amesema kuwa wanaushukuru mradi huo kwa kuwaelimisha juu ya shughuli za mashambani kupewa elimu ya shamba darasa kwa kufundishwa mbinu za kilimo hifadhi na kilimo rafiki.

No comments:

Post a Comment