Kijana mwenye umri wa miaka 21 Mkude Kulubuko anashikiliwa
na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka
11 anayesoma darasa la tatu katika shule ya msingi tangini.Tukio hilo limetokea
katika kijiji cha tangeni kata ya mzumbe, tarafa ya mlali , wilaya ya mvomero
mkoani morogoro ambapo mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo march 21 mwaka huu.
Akielezea tukio hilo babu wa mtoto aliye lawitiwa Charles Golaga
amesema kuwa march 21 mwaka huu mjukuu wake alikuwa akicheza na watoto wenzake
ndipo mtuhumiwa alipomrubuni na kwenda kumfanyia mnyama huo vichakani .
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha tangeni Joseph
Peter ameeleza kuwa amedhibitisha kuwa mtoto huyo amelawitiwa baada ya
kumpelekwa hospitalini na daktari kuweleza kuwa mtoto huyo amearibika sehemu
zake za haja kubwa na anamatatizo ya kujisaidia ovyo.
Aidha baba wa mtoto
huyo John Kesi Gabriel amekili kwa kutokea kwa tukio hilo ambaye amesema mwanae
anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa morogoro na hali yake
anaendelea vizuri.
Aidha kwa upande wa Kamanda wa Polisi mkoa Morogoro Faustine Shilogile alipotafutwa
kulizungumzia tukio hilo amesema kuwa hana taarifa zozote kwani yupo kikazi nje
ya mkoa morogoro.
No comments:
Post a Comment