Mkuu wa shule ya msingi kilosa town wilayani kilosa mkoani
morogoro mwalimu Edna Dungumaro ameupongeza mradi wa matokeo makubwa sasa [BRN]Kwa
kuweza kuinua kiwango cha ufaulu katika sekta ya elimu.
Hayo ameyasema march 18 alipotembelewa na habarikwanza
shuleni hapo na kusema kuwa kwa upande wa shule yake kwa mwaka jana 2013
matokeo yalikuwa mazuri kwa kufaulisha wanafunzi 67 kati ya wanafunzi 71 wa
darasa la saba na kueleza kuwa changamoto inayomkabili katika shule hiyo ni
wanafunzi kuwa watoro,Pia amesema kuwa shule yake imeshika nafasi ya kumi [10]kiwilaya.
Aidha Navy kareen Ndoeka ambaye ni mwanafunzi wa darasa la
sita katika shule hiyo ya kilosa town ameushukuru mpango huo wa matokeo makubwa
sasa [BRN]Kwani wameweza kupata elimu kwa kiasi kikubwa.
Naye Jaspine mswaki mwanafunzi wa darasa la saba katika
shule hiyo ya kilosa town ameupongeza mpango huo mwa matokeo makubwa sasa [BRN]Pia
amewaomba walimu kuendelea kuwafundisha kwa moyo ili wapate elimu iliyo
bora.
No comments:
Post a Comment