Mwnyekiti wa kitongoji cha Mbwamaji kata ya Magomeni Wilayani Kilosa Emmanuel
Mwendapole amewataka wakazi wa magomeni waishio mabondeni kuhama mapema kuepukana na mafuriko yatakayo
waathili katika makazi yao.
Kwa mujibu wa Mwendapole amesema kuwa kitongoji chake
kilivamiwa na maji mnamo march 29 na kuwaadhili wakazi 56 waishio katika kitongoji chake, Pia Mwendapole
ameiomba serikali kuwajengea tuta litakalo zuia maji , maji yatokayo
mtoni na kuvamia makazi ya watu pia
ameongeza kwa kusema kuwa anawataka wananchi kuacha kulima pembezoni mwa mto
huo wa mkondoa ili kujihami na mafuriko hayo.
Aidha wahanga hao wa mafuriko hayo Mohamedi Mungumbele na
Lussia Joseph wamesema kuwa mafuriko
hayo yameathili kuanzia mazao ya mashambani vyakula pamoja na mifugo. Na kusema
kuwa baadhi ya vitu vimeharibika ikiwemo vitanda na vyombo
No comments:
Post a Comment