Tuesday, August 5, 2014

WANANCHI WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO WALALAMIKA KUCHAKACHULIWA FEDHA ZAO



Wananchi wa wilayani kilosa mkoani morogoro wameilalamikia serikali kwa matumizi mabaya ya fedha zao za kodi ambazo zipo kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao na badala yake baadhi ya viongozi kutumia fedha hizo kwa manufaa yao binafsi.
                            Wananchi wakiwa katika barabara iliyofunguliwa na mh:waziri wa nchi ofisi ya waziri  mkuu tawala za mikoa TAMISEMI Hawa Ghasia

Baadhi ya wananchi hao khamisi juma na Bi,Aisha Salehe wamesema kuwa barabara hiyo yenye kiwango cha lami imetengenezwa bila ubora wowote kwani haijachukua muda tangu kukamilika kwake lakini kuna baadhi ya vipande vimeshaanza kubanduka.
Aidha wamesema kuwa baada ya ufunguzi wa barabara hiyo yenye kiwango cha lami yenye urefu wa km 0.9 inayokadiliwa kuwa imetumia kiasi cha shilingi milioni mia tatu 300 za kitanzania ambapo barabara hiyo imefunguliwa na julai 18 mwaka huu na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Hawa Ghasia. 
                                   Wananchi wakishuhudia barabara ikifunguliwa rasmi

Akijibu malalamiko hayo mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo amesema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusiana na ujenzi huo wa barabara kwa kusema kuwa watakuja wataalamu kwa ajili ya kuja kupima kiwango kilichojengwa katika barabara hiyo na kusema kuwa barabara hiyo imejengwa kwa kiwango cha kati na kuhusiana na ubora amewaambia wananchi kusubiri wakaguzi watakapo kuja kwa ajili ya kutoa majibu ya ujenzi wa barabara hiyo na ameongeza kuwa mpango huo wa ujenzi wa barabara ni mpango wa kuboresha mji wa kilosa kuwa katika muonekano mzuri  na ameongeza kuwa huo na mpango mwendelezo wa kuboresha barabara za mji huo wa kilosa.

VIONGOZI WILAYANI KILOSA WATAKIWA KUSIMAMIA WAFUGAJI KUTOINGIA KIHORELA WILAYANI KILOSA



Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo amewataka viongozi  wa vijiji kutowapokea wafugaji  wanaotoka maeneo ya vijiji vya  jirani na kuvamia katika maeneo ya wakulima.
Ameyasema hayo agost  4 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima wilayani kilosa mkoani morogoro na kusema kuwa katika wilaya yake kuna wafugaji wengi hivyo hahitaji tena wafugaji kutokana na wilaya hiyo kuwa na wafugaji wengi na kukwamisha shughuli nyingine za kimaendeleo.
Ameongeza kwa kusema kuwa viongozi waliopo vijijini wanawakaribisha wafugaji hao kwa kupewa rushwa na wanapoona mambo yanawashinda  huchukua hatua ya kuwafukuza na na kushindwa kutokana na rushwa ambayo wameshaipokea.
Pia amesema kuwa pindi atakapo baini kuwa kiongozi yeyote amepokea rushwa kwa ajili  ya kumkalibisha mfugaji katika eneo lake basi atakuwa amepoteza sifa ya kuwa kiongozi.
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa kilosa kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji kwa ajili ya kulinda ardhi na pia kuondoa migogoro.

Wednesday, July 23, 2014

VIJANA ZAIDI 100 WA CHADENA WILAYANI ULANGA WAJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM



 BAADHI YA VIJANA AMBAO NI AWALI WALIKUWA WANACHAMA WA CHADEMA WAKIONYESHA KADI ZAO MPYA ZA  CHAMA CHA MAPINDUZI  CCM


Vijana zaidi ya 100 ambao ni wanachama wa chama cha Demokrasia  na maendeleo  CHADEMA    wilaya ya Ulanga  mkoani Morogoro wamekihama chama hicho  na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).
Pamoja na vijana hao pia Viongozi wa juu wa chama hicho wilayani humo  wakiwemo Mwenyekiti wa wazee wa chadema ambaye  pia ni mjumbe wa halmashauri ya mkoa wa chama hicho ndugu Philipo Zimani na Kaimu mwenyekiti wa chadema jimbo la ulanga mashariki  ambaye pia ni katibu kata wa chadema kata ya ruaha wilayani humo Deodatus Charleswamekihama chama hicho na kujiunga na CCM.
MRATIBU WA WAZEE WA CHADEMA NDUGU ZIMANI  NA  KATIBU KATA WA CHAMA HICHO WILAYANI HUMO DEODATUS CHARLIES, WAKIKABIDHI BENDERA ZA CHAMA HICHO KWA UONGOZI WA CCM.
 
Hatua hiyo ya wanachama hao wa CHADEMA kujiunga na CCM imekuja kufauatia maendeleo mbalimbali yanatekelezwa na mbunge wa jimbo hilo la Ulanga Mashariki Serina Kombani, Kama vile ujenzi wa Barabara na ujenzi wa Soko.
Baadhi ya viongozi wa CCM na wale kutoka chama cha CHADEMA waliokiama chama hicho na kujiunga na CCM
Uwajibikaji wa viongozi wa serikali katika majukumu yao wilayani humo ni moja ya sababu inayowafanya wanachama wa vyama vya  upinzani kurudi chama cha mapinduzi  CCM.

WAZAZI NA WALEZI WANUFAIKA NA SHIRIKA LA HUDESA KATIKA KUPUNGUZA UDUMAVU WA WATOTO NA VIFO VYA KINAMAMA



Shirika lisilokuwa la kiserikali HUDESA linalofadhiliwa na USAID Kwa ushirikiano na AFRICARE linaendesha mafunzo ya lishe bora kwa kina mama wajawazito na wanaonyonyesha kwa lengo la kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka miwili wilayani kilosa mkoani morogoro. 


                           Afisa mradi ustawi wa HUDESA wilayani kilosa Hawa Hatibu

                                   Viazi lishe kwa ajili ya watoto na kinamama wanaonyonyesha

Akizungumzia malengo ya HUDESA julai 22 mwaka huu Afisa ustawi wa shirika hilo wilayani kilosa Hawa Hatibu amefafanua kuwa mwanzo bora ni siku elfu moja akiwa na maana toka motto yupo tumboni hadi kuzaliwa kwake na kufikia umri wa miaka miwili [2]ameeleza kuwa kitaalamu motto anapokosa lishe bora kwa kipindi hicho anaweza kudumaa kiakili na kimwili.
                                                          Bustani ya kiroba

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa katika mpango huo wa mwanzo bora wanafundisha kinamama jinsi ya kuandaa chakula bora kwa mtoto sambamba na hapo wameandaa bustani ya mbogamboga za majani pamoja na viazi lishe ambavyo hutumika kumuandalia chakula mtoto.
                                     Baadhi ya walezi wakiwa kwenye bustani
Kwa upande wake Salehe kaombwe ambaye na mhudumu wa afya wa majumbani kata ya kasiki wilayani kilosa amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuepukana na vifo vya kinamama na udumavu wa watoto.
                                              Bustani ya mbogamboga aina ya chainizi

Nao baadhi ya kinamama wa wilayani kilosa mkoani morogoro Husna Rashidi na Amina bint Ally wamesema kuwa wanalishukuru sana shirika la HUDESA kwa kuwapatia elimu ya mafunzo ya jinsi ya kuwaandalia lishe iliyobora watoto wao ili waweze kukua vizuri na kuweza kuepukana na magonjwa yanayoepukika.



Friday, July 18, 2014

HAWA GHASIA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Mheshimiwa Hawa Ghasia amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa kusimamia vizuri vyanzo vya mapato vilivyopo Wilayani humo  ili kuleta maendeleo na kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili. 
     waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI)Hawa Ghasia     akifungua barabara ya lami inayoelekea ofisi za halmashauri ya wilaya ya kilosa

Ghasia amesema hayo Julai 18 mwaka huu  alipokuwa kwenye mkutano maalumu na watumishi pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo kwenye ziara yake  ya siku moja  wilaya ya kilosa yenye lengo la kukagua na kuzindua miradi mbambali ya maendeleo wilaya ya kilosa mkoani morogoro.
            Baadhi ya wananchi waliohudhulia katika ufunguzi wa barabara ya lami inayoelekea  ofisi za halmashauri ya wilaya ya kilosa

Ghasia amesema kuwa endapo vyanzo vya mapato vitasimamiwa vyema Halmashauri itakuwa na uhakika wa kupata mapato ya kutosha ambayo yataweza kusaidia kununua magari kwa ajili ya matumizi ya maendeleo kwa Halmashauri na mahitaji mengine pia kuhakikisha inatatua changamoto ya uwepo wa Makaimu Wakuu wa Idara kwa kuteua Watendaji wenye sifa ili kuwa na uadilifu katika shughuli za kiutendaji.
              Maafisa usalama nao hawakuwa nyuma kuhakikisha shughuli zote zinakamilika kwa amani

Sambamba na hayo katika ziara yake ya siku moja Wilayani Kilosa Ghasia amepata wasaha wa kuzindua Barabara ya lami Bomani na Hospitali ya Wilaya,Mradi wa wodi ya wagonjwa grade two na ukarabati wa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Wilaya,Mradi wa Kilimo Shadidi na kupokea taarifa ya mradi wa upimaji viwanja vya wahanga wa mafuriko Tarafa ya Magole pia amewasisitiza Madiwani na Watendaji wa Halmashauri kusimamia mapato na kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata taratibu zote za kazi.

Saturday, July 12, 2014

WATUMISHI WA AFYA WATAYEBAINIKA KUWAUZIA WAGONJWA DAMU KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA

















Jamii imetakiwa kuwa na ushirikiano na wahamasishaji  wa damu salama ili kuwabaini  na kuwachukulia hatua kali za kisheria watumishi wa afya watakaobainika kutumia vibaya damu inayotolewa na wananchi kwa kuwauzia wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

Hayo yamebainishwa mkoani morogorogo katika mafunzo ya uhamasishaji wa mpango wa taifa wa kuchangia damu salama na Afisa uhamasishaji Bernadino Medaa, na kusema kuwa  suala la uuzaji wa damu sio suala la kupambana na  mpango wa Damu Salama pekee bali la wananchi wote kwa pamoja kushirikiana  kulitokemeza kabisa jambo la uuzaji wa damu wagonjwa wanaohitaji.

Ili kutokomeza tabia hiyo, Afisa  Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Damu salama, nchini Bernadino Medaa ameitaka jamii kuwa na ushirikiano na shirika la Damu salama ili kuweza kuwadhibiti waharifu hao ambao ni watumishi wa afya wanauza damu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.















Kwa upande wake Afisa  mahusiano wa mpango wa taifa wa damu salama, Rajabu Mwenda amewataka watumishi hao wa afya kuacha mara moja tabia ya kuwauzia wagonjwa wanaohitaji huduma ya Damu, kwani kufanya hivyo kunakatisha tama a kwa wananchi kushindwa kuijitokeza kuchangia huduma hiyo ya Damu.

Baadhi ya wahamasishaji wakiwa makini katika mafunzo hayo














 \
















Nao Washiriki wa mafunzo hayo Lacas Michael, Afisa uhamasishaji kanda ya Mashariki na na Evelyne Kussaga, afisa masoko wa Mpango wa Taifa wsa Damu salama, wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa wa ukusanyaji wa damu salama  hasa mashuleni ambao wanafunzi ndio wadau wakubwa wa ukusanyaji damu nchini .

Mafunzo hayo yamedumu kwa muda wa siku sita ambayo yameanza tarehe 6 mpaka tarehe 12 mwezi huu, ukiwakutanisha wahamasishaji wa damu salama na watumishi wa afya kote walipo nchi kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya umasishaji wa utoaji wa damu salama kwa wananchi.