Friday, July 18, 2014

HAWA GHASIA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Mheshimiwa Hawa Ghasia amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa kusimamia vizuri vyanzo vya mapato vilivyopo Wilayani humo  ili kuleta maendeleo na kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili. 
     waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI)Hawa Ghasia     akifungua barabara ya lami inayoelekea ofisi za halmashauri ya wilaya ya kilosa

Ghasia amesema hayo Julai 18 mwaka huu  alipokuwa kwenye mkutano maalumu na watumishi pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo kwenye ziara yake  ya siku moja  wilaya ya kilosa yenye lengo la kukagua na kuzindua miradi mbambali ya maendeleo wilaya ya kilosa mkoani morogoro.
            Baadhi ya wananchi waliohudhulia katika ufunguzi wa barabara ya lami inayoelekea  ofisi za halmashauri ya wilaya ya kilosa

Ghasia amesema kuwa endapo vyanzo vya mapato vitasimamiwa vyema Halmashauri itakuwa na uhakika wa kupata mapato ya kutosha ambayo yataweza kusaidia kununua magari kwa ajili ya matumizi ya maendeleo kwa Halmashauri na mahitaji mengine pia kuhakikisha inatatua changamoto ya uwepo wa Makaimu Wakuu wa Idara kwa kuteua Watendaji wenye sifa ili kuwa na uadilifu katika shughuli za kiutendaji.
              Maafisa usalama nao hawakuwa nyuma kuhakikisha shughuli zote zinakamilika kwa amani

Sambamba na hayo katika ziara yake ya siku moja Wilayani Kilosa Ghasia amepata wasaha wa kuzindua Barabara ya lami Bomani na Hospitali ya Wilaya,Mradi wa wodi ya wagonjwa grade two na ukarabati wa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Wilaya,Mradi wa Kilimo Shadidi na kupokea taarifa ya mradi wa upimaji viwanja vya wahanga wa mafuriko Tarafa ya Magole pia amewasisitiza Madiwani na Watendaji wa Halmashauri kusimamia mapato na kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata taratibu zote za kazi.

No comments:

Post a Comment