Saturday, July 12, 2014

WATUMISHI WA AFYA WATAYEBAINIKA KUWAUZIA WAGONJWA DAMU KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA

















Jamii imetakiwa kuwa na ushirikiano na wahamasishaji  wa damu salama ili kuwabaini  na kuwachukulia hatua kali za kisheria watumishi wa afya watakaobainika kutumia vibaya damu inayotolewa na wananchi kwa kuwauzia wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

Hayo yamebainishwa mkoani morogorogo katika mafunzo ya uhamasishaji wa mpango wa taifa wa kuchangia damu salama na Afisa uhamasishaji Bernadino Medaa, na kusema kuwa  suala la uuzaji wa damu sio suala la kupambana na  mpango wa Damu Salama pekee bali la wananchi wote kwa pamoja kushirikiana  kulitokemeza kabisa jambo la uuzaji wa damu wagonjwa wanaohitaji.

Ili kutokomeza tabia hiyo, Afisa  Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Damu salama, nchini Bernadino Medaa ameitaka jamii kuwa na ushirikiano na shirika la Damu salama ili kuweza kuwadhibiti waharifu hao ambao ni watumishi wa afya wanauza damu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.















Kwa upande wake Afisa  mahusiano wa mpango wa taifa wa damu salama, Rajabu Mwenda amewataka watumishi hao wa afya kuacha mara moja tabia ya kuwauzia wagonjwa wanaohitaji huduma ya Damu, kwani kufanya hivyo kunakatisha tama a kwa wananchi kushindwa kuijitokeza kuchangia huduma hiyo ya Damu.

Baadhi ya wahamasishaji wakiwa makini katika mafunzo hayo














 \
















Nao Washiriki wa mafunzo hayo Lacas Michael, Afisa uhamasishaji kanda ya Mashariki na na Evelyne Kussaga, afisa masoko wa Mpango wa Taifa wsa Damu salama, wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa wa ukusanyaji wa damu salama  hasa mashuleni ambao wanafunzi ndio wadau wakubwa wa ukusanyaji damu nchini .

Mafunzo hayo yamedumu kwa muda wa siku sita ambayo yameanza tarehe 6 mpaka tarehe 12 mwezi huu, ukiwakutanisha wahamasishaji wa damu salama na watumishi wa afya kote walipo nchi kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya umasishaji wa utoaji wa damu salama kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment