Wananchi wa wilayani kilosa mkoani morogoro wameilalamikia
serikali kwa matumizi mabaya ya fedha zao za kodi ambazo zipo kwa ajili ya
maendeleo ya nchi yao na badala yake baadhi ya viongozi kutumia fedha hizo kwa
manufaa yao binafsi.
Wananchi wakiwa katika barabara iliyofunguliwa na mh:waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa TAMISEMI Hawa Ghasia
Baadhi ya wananchi hao khamisi juma na Bi,Aisha Salehe
wamesema kuwa barabara hiyo yenye kiwango cha lami imetengenezwa bila ubora
wowote kwani haijachukua muda tangu kukamilika kwake lakini kuna baadhi ya vipande
vimeshaanza kubanduka.
Aidha wamesema kuwa baada ya ufunguzi wa barabara hiyo yenye
kiwango cha lami yenye urefu wa km 0.9 inayokadiliwa kuwa imetumia kiasi cha
shilingi milioni mia tatu 300 za kitanzania ambapo barabara hiyo imefunguliwa
na julai 18 mwaka huu na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa na
serikali za mitaa TAMISEMI Hawa Ghasia.
Wananchi wakishuhudia barabara ikifunguliwa rasmi
Akijibu malalamiko hayo mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo
amesema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusiana na ujenzi huo wa barabara
kwa kusema kuwa watakuja wataalamu kwa ajili ya kuja kupima kiwango kilichojengwa
katika barabara hiyo na kusema kuwa barabara hiyo imejengwa kwa kiwango cha
kati na kuhusiana na ubora amewaambia wananchi kusubiri wakaguzi watakapo kuja
kwa ajili ya kutoa majibu ya ujenzi wa barabara hiyo na ameongeza kuwa mpango
huo wa ujenzi wa barabara ni mpango wa kuboresha mji wa kilosa kuwa katika
muonekano mzuri na ameongeza kuwa huo na
mpango mwendelezo wa kuboresha barabara za mji huo wa kilosa.
No comments:
Post a Comment