Mkuu wa
wilaya ya kilosa Elias Tarimo amewataka viongozi wa vijiji kutowapokea wafugaji wanaotoka maeneo ya vijiji vya jirani na kuvamia katika maeneo ya wakulima.
Ameyasema
hayo agost 4 mwaka huu wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na wafugaji kuvamia
maeneo ya wakulima wilayani kilosa mkoani morogoro na kusema kuwa katika wilaya
yake kuna wafugaji wengi hivyo hahitaji tena wafugaji kutokana na wilaya hiyo
kuwa na wafugaji wengi na kukwamisha shughuli nyingine za kimaendeleo.
Ameongeza
kwa kusema kuwa viongozi waliopo vijijini wanawakaribisha wafugaji hao kwa
kupewa rushwa na wanapoona mambo yanawashinda
huchukua hatua ya kuwafukuza na na kushindwa kutokana na rushwa ambayo
wameshaipokea.
Pia amesema
kuwa pindi atakapo baini kuwa kiongozi yeyote amepokea rushwa kwa ajili ya kumkalibisha mfugaji katika eneo lake basi
atakuwa amepoteza sifa ya kuwa kiongozi.
Aidha ametoa
wito kwa wakazi wa kilosa kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya
wakulima na wafugaji kwa ajili ya kulinda ardhi na pia kuondoa migogoro.
No comments:
Post a Comment