Shirika la world vision lililoanzishwamwaka 1959 nchini marekani
na kuingianchini Tanzania mwaka 1980 lenyelengo la kuleta ustawi wa motto kuwa na
maisha mazuri, Afya njema na kumjua mungu , May 20 mwaka huu limetoa mafunzo ya
ujasiriamali kwa vikundi vya vikoba wilayani kilosa.
Katika mafunzo hayo yaliyohudhuliwa na wajumbe kutoka katika
vikundi mbalimbali katika kutoa mafunzo hayo wamewezeshwa jinsi ya kuendesha vikundi
vyao na taratibu na kanuni za kufuata katika kuendesha vikundi vyao.
NayemenejawamradiwaUlaya ADP katikashirikala world vision Mathias Mwingila
amesema kuwa katika kutoa mafunzo hayo
MWEZESHAJI AKITOA MAFUNZO YA UJASILIAMALI KATIKA UKUMBI WA MANYOVU - KILOSA
Wanakumbana nachangamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanavikundi
kudai posho wakati wanapoitwa kupewa mafunzo na kusema kuwa lengo la world
vision nikutoa mafunzo ya kuweza kujikwamua kimaisha na kuleta maendeleo katika
jamii.
Aidha ameongeza kuwa changamoto nyingine ni mapokeo hasi
kwa baadhi ya wajumbe wakidhani kuwa world vision inaeneza dini ya kikristo
kutokana na shirika hilo kuanzishwa na watu wa dini ya kikristo na amebainisha kuwa
shirika hilo halipo upande wowote wakidini ila lipo kwaajili ya kutoa mafunzo ya
kujikwamua kimaisha kwa wajasiriamali wadogowadogo.
WANAVIKUNDI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA MAFUNZO .
Nameongeza kuwa mradi huo kwasasa upo katika tarafa ya ulaya
na Magole na utachukua muda wamiaka kumi na mitano na mikakati waliyojiwekea nikuhakikisha
wajasiriamali na wananchi kwaujumla wanapata maendeleo kwa haraka.
Pia mwezeshaji katika semina hiyo Agripina P. Mtende amewataka
wanavikundi hao kuwa na nidham ya fedha pindi wanapokopa katika vikundi vyao.
Baaadhi ya wanavikundi hao Mwanaharusi Athumani, Donard Kusema
na Stamili Shabani Kiwanga wamesema kuwa wameshukuru kwa shirika hilo la world vision kwa kuwapatia elimu hiyo juu ya
uendeshaji wa vikundi vyao.