Mkaguzi mkuu wa shule wilayani kilosa Ally Abdulhaman
amewataka wadau wa elimu kufuata kanuni na taratibu za kuanzisha shule pamoja
na vyuo.
Ameyasema hayo ofisini kwake wakati akizungumzia usajili wa
Snai Media school iliyopo manzese wilayani kilosa na kusema kuwa shule hiyo
haikusajiliwa tangu ilipoanzishwa mwaka 2009 na kusema kuwa walishatoa
maelekezo kwa mmiliki wa shule hiyo kuwa ataje usajili wa shule hiyo mapema na
kuongeza kuwa shule hiyo iliamuliwa kufungwa na mkaguzi wa mkoa mnamo tar 31
january lakini shule hiyo bado inaendelea kutoa mafunzo hayo ya elimu.
Aidha amesema kuwa wahisani hao huanzisha shule hizo kwa
kupitia ofisi ya ustawi wa jamii yaani child care lakini ndani yake hutoa elimu
ambapo ni kinyume na taratibu na sheria na kubainisha kuwa watoto kuanzia umri
wa miaka 0 hadi 4 ndio wanaotakiwa kuwa kwenye child care na wanapofikia umri
wa miaka 5 huyo anakuwa na umri wa kuanza elimu ya awali.
Naye mkurugenzi wa Snai media school Mery Paul Komba amesema
kuwa shule yake ipo kwenye mchakato wa kuisajili likini pia amesema kuwashule
hiyo bado ipo chini ya ustawi wa jamii na wapo kwenye mpango wa kuisajili
lakini serikali inawapelekesha haraka na wanashindwa cha kufanya kwa sababu
wanachanganywa na kuongeza kuwa swala la kufungwa kwa shule hiyo limewaumiza
sana wazazi wenye watoto katika shule hiyo na kueleza kuwa elimu wanayoipata
watoto katika shule hiyo ni nzuri na wanaumizwa wanapooona shule hiyo inataka
kufungwa.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa lengo la kuanzisha shule
hiyo ni kutokana na kuona kiwango cha elimu kinashuka na changamoto kubwa na
swala la lugha ya kiingereza.
Nao wanafunzi katika shule hiyo ya Snai media school shurut
palma na careen fredy wamesema kuwa changamoto inayowakabili shuleni hapo ni
kutokuwepo maji kalibu pia vyoo kutofanyiwa usafi ulio sahihi kwa usalama wao.
No comments:
Post a Comment