Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk Mohamed
Gharib Bilal amewataka watanzania kuwa wazalendo na nchi yao kwa kufichua
vitendo vya rushwa vinavyoendelea kukithili nchini.
Ameyasema hayo katika
uzinduzi wa mbio za mwenge uliozinduliwa rasmi 2may katika mkoa wa kagera
wilayani bukoba katika viwanja vya
kaitaba wenye kauli mbiu isemayo Tujitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba
bora na kusema kuwa rushwa ni chanzo cha
kufifia kwa maendeleo kwa kuathili kila sekta na kusema kuwa watanzania wote
tushirikiane katika kutokomeza rushwa na kusema kuwa jukumu la kutokomeza
rushwa si jukumu la Taasisi ya kupambana na kutokomeza rushwa TAKUKURU peke
yake bali sote tushirikiane katika kupambana na rushwa .Pia ameeleza sababu ya
rushwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili,tama ya kujilimbikizia mali na
kukosekana kwa uzalendo.Na kutoa Rai kwa watanzania kuacha kutoa na kupokea
rushwa na wanapoona vitendo hivyo walipoti taarifa mapema kwa mamlaka
husika.
Naye Waziri wa habari vijana tamaduni na michezo Fenera
Mkangara amesema kuwa mwenge wa uhuru ni tunu na ishara ya uhuru wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania pia amesema kuwa mwenge wa uhuru ni unatumika kuchochea
maendeleo kwa wananchi kwani wananchi huamasishwa kubuni na kuandaa miradi
mbalimbali ya kijamii na uchumi.
Aidha amesema kuwa kwa mwaka huu mwenge wa uhuru utakimbizwa
kwa siku 165 katika halmashauri za wilaya zote za Jamhuri ya muungano wa
Tanzania na kusema kuwa mbio hizo za mwenge zinatarajiwa kifikia tamati katika
mkoa wa Tabora tarehe 14 October 2014 na atakayehitimisha mbio hizo za mwenge
ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment