Umoja wa katiba ya wananchi [UKAWA]Wameendelea kuwahamasisha
wananchi juu ya umuhimu wa katiba na ukawa walivyojitoa kwenye bunge maalum la
katiba wakipinga mabadiliko yanayotarajiwa toka kwa kamati na kanuni,wakidai
kuwa yanaenda kinyume na azimio lililopitishwa na bunge hilo kwa kuleta maridhiano.
Akiongea katika mkutano ulioitishwa na UKAWA katibu wa chama
cha CUF wilayani kilosa Sudy muhombolage amesema kuwa sababu ya ukawa kujitoa katika
bunge maalum la katiba ni Lugha za kibaguzi,Vitisho vilivyojitokeza katika
bunge maalum la katiba pamoja na kuchakachua kwa rasimu ya katiba kwa baadhi ya
wajumbe wa bunge hilo la katiba.
Naye kamanda wa chama cha demokrasia na maendeleo [chadema]
mkoa wa morogoro Abdalah Hamisi amesema kuwa msimamo wa Ukawa ni serikali tatu
na kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa serikali tatu,Pia ameongeza kwa
kusema kuwa Ukawa wanania nzuri na wananchi lakini kuna baadhi ya vyama
wanamsimamo wa kivyama na ndio wanaosababisha mgogoro bungeni kwa kupingana na
maoni ya wananchi ambayo yalikusanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba
No comments:
Post a Comment