Wafanyabiashara wa mazao pamoja na nguo mnada wa Lumuma
wilayani kilosa mkoani morogoro may 1 wametekwa na kuporwa mali zao na
kujeruhiwa katika eneo la la mlima wa vua shati uliopo barabara ya lumuma
wilayani kilosa.
Wafanyabiashara
hao waliotekwa akiwemo Blai jaston na David Daudi komba wametekwa katika mlima
wa vua shati na majambazi waliokuwa wakitumia silaha aina ya mapanga na
Nondo,Kati ya bidhaa zilizotekwa na majambazi hao ni pikipiki aina ya sanlg yenye
namba za usajili T 210PVA Iliyokuwa ikimilikiwa na msafiri mkazi wa mpwapwa na
bidhaa nyingine zilizotekwa ni pamoja na nguo sambamba na maharage.Akielezea
tukio hilo mmoja wa mateka hao bw,jaston amesema kuwa walitekwa may 1 majira ya
saa 3 usiku eneo la mlima wa vua shati na kufungwa kamba za mpira na kuamrisha
kutowaangalia usoni na kuamrishwa watoe vitu walivyonavyo ikiwemo fedha walizopata
katika mauzo waliyouza kwa siku hiyo na walipokataa ndipo walipoanza kupingwa
na nondo na hatimaye kukatwa mapanga.
Aidha mmoja
wa ndugu wa majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Baba Maria Okocha amesema
kuwa eneo hilo walipotekewa ni sehemu mbaya kwani kuna mlima mkali na
maporomoko na kusema kuwa nyia hiyo ni hatari kwani hakuna watu wapitao mara
kwa mara na kuongeza kuwa majambazi hao waliangusha mti barabarani wakiwavizia
watu wanaorudi kutoka mnadani.
Kwa mujibu
wa kaka wa majeruhi Sita Komba amesema kuwa
mdogo wake aitwaye David alikatwa mapanga eneo la kichwa na walimpeleka
wamempeleka hospital wakipitia polisi kupata PF3 Na kueleza kuwa kwa sasa
anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibubu.
Naye kamanda
mkuu wa wilaya ya kilosa SP Break M.Magesa [OCD]amethibitisha kuwa tukio hilo limetokea
eneo la vua shati kwa tukio la majambazi kupora pikipiki na mali za wafanya
biashara hao na kutoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi
ili kubaini wahalifu wanaojaribu kujiinua.
No comments:
Post a Comment