Waliokuwa wanachama wa chama cha kupanda na kuvuna DECI Wilayani Kilosa wameoiomba
serikali iwarejeshee pesa zao kama ilivyowaahidi au itoe tamko lolote juu ya
pesa zao ili wafahamu kinachoendelea.
Wakizungumza
na HABARIKWANZA baadhi ya wanachama hao wamesema serikali imekaa kimya kwa muda mrefu kitu ambacho
kinawapa wasiwasi wa kurejeshewa pesa zao kama serikali ilivyowaahidi.
Mmoja wa
wanachama hao Nassoro Machengo ambaye alipanda zaidi ya milioni moja amesema
baada ya serikali kuthibitisha na kuifungia taasisi hiyo na kuipeleka
mahakamani ili ahidi kurejesha pesa kwa wananchi waliopanda ambacho
wanavielelezo mara tu kesi hiyo itakapokamilika .
Machengo amesema
wanashangazwa na ukimya wa serikali wakati kesi imeshakamilika na serikali
imeshindwa kufanya hivyo wanaomba serikali iwarudishie pesa kama ilivyo ahidi
au itoe tamko lolote juu ya kinachoendelea kwa kukaa kwao kimya kinawapa
wasiwasi na kuhisi kuwa hawatapata tena pesa hizo .
Takribani miaka
7 iliyopita kuiibuka taasisi ya kifedha ya DECI iliyokuwa ikijiendesha katika
utaratibu wa kupanda na kuvuna pesa ambapo wananchi mbalimbali waliwekeza pesa
kwa lengo la kuvuna pesa zaidi , lakini
taasisi hiyo ilikuwa ikiendeshwa kinyume na taratibu za kisheria hivyo serikali
ilisimamisha kufanya shughuli hizo huku ikiwa imekusanya mabilioni ya watanzania.
No comments:
Post a Comment