Sunday, February 23, 2014

AJALI MBAYA YA MOTO YATOKEA MIKESE MKOANI MOROGORO LEO ASUBUHI.

 



 Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka
Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto huo

  Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana  na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Peter Laurence

Friday, February 21, 2014

RT WAWASILISHA MAJINA 40 YA WANARIADHA KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE.

Shirikisho la Riadha Tanzania limewasilisha majina 40 ya wanariadha na sita ya walimu kwenye ofisi ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa tayari kwa ajili ya timu ya taifa ya riadha  kushiriki katika  mafunzo  nje ya nchi.

Rais wa shirikisho la riadha Tanzania Anthony Mtaka amesema wameamua kuwasilisha majina hayo mara baada ya wizara hiyo  kuchukua jukumu la kuwapeleka wanariadha hao nje ya nchi kwenda kujifunza ili baadaye waiwakilishe vema nchi katika mashindano ya Kimataifa.

Wednesday, February 19, 2014

WADAU MBALIMBALI WAHIMIZWA KUENDELEA KUTOA MISAADA KUWASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MKOANI MOROGORO.


Serikali Mkoani Morogoro imefanikiwa kujenga mahema 330 katika vijiji viwili vilivyoathirika na Mafuriko katika wilaya ya Kilosa na Mvomero, ambavyo ni Magore na Mateteni, huku lengo la serikali likihitaji kujenga mahema 520 ili kumuwezesha kila wananchi kuwa na sehemu yake ya kuishi.

Friday, February 14, 2014

KIVUMBI CHA LIGI DARAJA LA KWANZA KUENDELEA KUTIMKA KESHO KATIKA VIWANJA TOFAUTI NCHINI


( PICHA BY PETER LAURENCE )
                                            
Timu ya polisi Morogoro imeondoka jana kuelekea Iringa ikiwa tayari kwa mchezo wa ligi daraja la kwanza  dhidi ya LIPULI ya mkoani humo,  mchezo utakaochezwa jumamosi ya Februari 15 katika uwanja wa Samora Iringa.

MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA YA KILOSA AMETAKIWA KUWAITA WALIMU ILI KUWAELEZA UKWELI WA MATATIZO YAO.


Mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya wilaya ya kilosa masalu mayaya,ametakiwa kuwaita walimu wote wa wilaya ya kilosa ili kuweza kuwaeleza matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.

Wito huo umetolewa Februari 13 mwaka huu na mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya kilosa mheshimiwa Amer Mubarak katika kikao cha kamfed kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo wakati kamfed ilipokuwa ikikabidhi vitabu vya wanafunzi wa sekondari .
Mubarak emesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kujua matatizoyanayowakabili na kuyatafutia ufumbuzi,lengo likiwa ni kuongeza ufaulu mashuleni.
Pia amezitaka bodi za shule kuwa makini nakupa ulewa  wa matatizo yashule zao na kujaribu kutatua na ikishindikana wafike wilayanikuomba nsaada.
;
Aidha mwenyekiti wa halmashuri hiyo ametaka wananchi wahamasishwe kujenga nyumba za walimu karibu na shule ili kuwapa wepesi katika kufanya kazi yao ya kufundisha.

WILAYA YA KILOSA NA WILAYA MPYA YA GAIRO WAMEPOKEA MSAADA WA VITABU AROBAINI NA SABA ELFU NA THELATHINI


      Jumla ya vitabu arobaini na saba elfu na thelathini February 13 mwaka huu  vimetolewa kwa shule za sekondari  wa kumi na tisa wilayani kilosa na shule sita wilaya mpya ya Gairo.

      Vitabu hivyo vimetolewa na shirika la camfed ambalo linashughulikia kwa kuwasaidia watoto walio mashuleni wasio na uwezo licha ya kutoa vitabu na vifaa vingine mashuleni ,pia shirika hilo hutoa karo za shule na mavazi kwa wanafunzi hao.
        Akikabidhi vitabu hivyo kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilosa Amer  Mbaraka Afisa mradi wa kamfed ambaye pia ni mlezi wa kafed mkoani morogoro Deogratius john amesema kuwa kamfed imedhamilia  Nyanja ya elimu ili kufanikisha mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa  yaani [BRN].
         Kati ya vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Dunia yangu bora,How to read English,English study guide,mathematical study guide na biology studyguide
Pia bwana Deogratius John amewataka walimu kupanga mkakati bora kwa kila mwanafunzi apate vitabu hivyo na kuvitumia ipasavyo.

Thursday, January 9, 2014

Mbunge wa jimbo la kilosa atembelea miradi mbalimbali katika jimbo lake

        Mbunge wa jimbo la kilosa Mustafa Haidi mkulo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezajiwa miradi ya maendeleo katika kata za Lumuma na kidete wilayani klilosa.
        Akiwa katika ziara hiyo,Mkulo aliongozana na katibu wa wazazi wilaya  Abdul Gombe na wataalamu mbalimbali kutoka wilaya ya kilosa.
         Katika kata ya kidete Mbunge mkulo amekagua mradi wa ujenzi wa bwawa la kidete ambalo hadi sasa halijakamilika tangu mwaka 2010 ulipoanza,Sababu ikiwa ni kutowaingizia pesa inayosimamia mradi huo wa ujenzi wa bwawa.
         Aidha amekagua mradi wa uchongaji wa barabara wa lumuma-kibasingwa yenye urefu wa kilometa nane ambayo imechongwa kilometa sita hadi sasa barabara hiyo imechongwa na mfuko wa jimbo wa mkulo,ambapo mbunge huyo ameahidi kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia kilometa mbili zilizobaki.
Mbunge mkulo amefanya ziara hiyo January 6 n January7 ambapo pia ameweza kutembelea mradi wa barabara ya lumuma Mnozi ambayo haijakamilika hadi sasa na mbunge huyo ameahidi kuwa barabara hiyi itaanza kuchongwa mapema hivi karibuni.
         

Friday, January 3, 2014

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA CHANZURU KINATARAJIA KUKUSANYA MILIONI THELATHINI NA MOJA LAKI TATU NA AROBAINI ELFU



Halmashauri ya kijiji cha chanzuru wilayani kilosa mkoani morogoro inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi milioni Thelathini na moja laki tatu na arobaini elfu kwa ajili ya maendeleo ya kijiji.
Hayo yamesemwa mapema mwanzoni mwa wiki hii na mtendaji wa kijiji hicho salumu kibugula wakati akiongea kwenye mkutano wa wananchi na viongozi wa kijiji hicho alipokuwa akisoma bajeti ya mapato na matumizi ya nusu ya mwaka wa fedha 2013/2014.
Kibagula amesema kuwa katika bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2013/2014 kijiji kinatakiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni ishirini na moja laki tatu na Arobaini kupitia vyanzo vyake vya ndani na shilingi milioni kumi kutoka kwa wahisani na ruzuku ya halmashauri ya wilaya kilosa.
Katika mkutano huom pia kumejadiliwa mgogoro wa mashamba kati ya mwekezaji aliyefahamika kwa jina la Bahamisi na wananchi wa kijiji hicho kuhusiana na mipaka iliyowekwa na idara ya ardhi wilayani kilosa

VIJANA WATAKIWA KUUNDA VIKUNDI ILI WAPATE MIKOPO KIURAHISI



Mbunge wa jimbo la mikumi mkoani morogoro Abdulsalama Amer amewataka vijana waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama bodaboda kuunda vikundi ili waweze kupatiwa mkopo wa pikipiki zitakazowawezwsha kujikwamua kiuchumi.
Abdulsalama maarufu kwa jina la sas gesametoa wito huo kwa vijana wa jimbo lake la mikumi wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha kitete msindazimapema wiki hii wakati wa ziara yake kwenye kijiji hicho kilichopo kwenye kata ya Ruhembe wilayani kilosa.
Sas gas amesema kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na kampuni husika itakayotoa mikopo hiyo na sasa kinachosubiriwa ni vijana hao kuunda vikundi na kufuata taratibu zinazotakiwa ili waweze kukopeshwa.
Mbunge huyo amesema mikopo hiyo itawasaidia vijana hao kupata pikipiki na wataweza kuacha kuendesha pikipiki za matajiri wao na kuendesha za kwao kitu ambacho kitawasaidia kijikwamua kiuchumi.
Wakiongea vijana hao wamesema kuwa wanampongeza mbunge wao kwa jitihada hizo kwani watakapokopeshwa hizo pikipiki zitawasaidia kupata pesa na kuweza kutimiza ndoto zao za maisha bora kwa upande wao.

Wednesday, December 18, 2013

Anusurika kuuawa na majambazi wilayani kilosa

Mkazi wa manispaa ya wilaya ya kilosa mkoani morogoro,costa mwamba amenusurika kuuawa baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wanaosadikiwa ni majambazi.


Akizungumzia tukio hilo mtendaji wa kijiji cha munisagara Donald mgulambwa amesema kuwa tukio hilo limetokea dec 17 mwaka huu majira ya saa nane usiku ambapo watu hao walifika nyumbani kwa bwana mwamba na kuvunja mrango kwa jiwe maarufu kama jiwe Fatuma.,
Amesema kuwa majambazi hao ambao wanasadikiwa kuwa ni wane baada ya kufanikiwa kuvunja mlango huo waliingia ndani na ndipo walipoanza kumcharanga kwa mapanga bwana mwamba pamoja na mkewe Chiku Salumu na kasha kufanikiwa kuchukua kiasi cha pesa shilingi laki nane.

Mgulambwa amesema kuwa baada ya majambazi kufanya uhalifu huo majeruhi hao walipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani ndipo majambazi hao wakatokomea kusiko julikana.

Majirani wa eneo hilo walimkimbiza bwana Mwamba katika hospitari ya wilaya ya kilosa kutokana na majeruhi makubwa aliyoyapata huku mkewe akipelekwa katika katika zahanati ya kijiji hicho.

Tukio kama hili ni la pili kutokea katika kijiji cha munisagara ambapo viongozi wa kijiji viongozi wametoa taarifa katika kituo cha polisi wilani kilosa kwa uchungzi zaidi.

Thursday, December 12, 2013

VIKUNDI VYA POLISI JAMII VYAPEWA VITAMBULISHO WILAYANI KILOSA


Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya kilosa peter nsato [SP]Dec 12 ametoa vitambulisho kwa vikundi vya polisi jamii wilayani kilosa.

 Mgeni rasmi SP Peter Nsato akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa vikundi vya polisi jamii Wilayani Kilosa.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya kilosa peter nsato [SP] amevitaka vikundi vya polisi jamii wilayani humo kutenda kazi kwa uadilifu na kuwataka kufichua uhalifu punde unapotokea,Pia katika kuwapatia vitambulisho  wanavikundi hao wamepewa mavazi ya kujitambulisha kuwa askari [reflector]pindi wawapo kazini.
 Matanda Ally matanda akipokea mavazi ya polisi jamii kutoka kwa SP Peter Nsato mara baada ya kupokea kitambulisho

 Aidha mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya kilosa [ASP]Antony mkwawa amesema kuwa jeshi la polisi limeamua kuanzisha uhamasishaji wa polisi jamii na ulinzi shilikishi lengo likiwa ni kupungunza uhalifu unaotokea katika jamii na kulinda mali za wananchi,Na kuongeza kuwa jeshi la polisi linauhaba wa polisi na kuwataka wananchi kushirikiana vizuri na polisi jamii hao ili kumaliza kabisa matukio ya kiharifu yanayotokea katika jamii.            
 
       
 Aliyesimama ni mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya kilosa ASP Antony mkwawa na wapili Kushoto kwake ni SP  Peter Nsato.

Aidha katika risala iliyoandaliwa katika vikundi hivyo ambavyo ni UKOMBOZI ULINZI SHIRIKISHI Kutoka kata ya kasiki,MALIWASO ULINZI SHIRIKISHI kata ya mbumi na MTENDENI B ULINZI SHIRIKISHI,Wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuwashirikisha wanajamii kwani imesaidia kuvumbua matatizo yaliyopo kwenye jamii.
                 Hata hivyo wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi kama vile tochi,usafiri,makoti kwa ajili ya mvua na kuliomba jeshi la polisi tarafa ya kilosa liendelee kuwahamasisha wadau mbalimbali katika maeneo yao kuvisaidia vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi.